Kuna hitilafu kwenye distribution and value chain ya vyakula nchini mwetu. Hasa upande wa supply. Kwangu mie, huu ni mfano mzuri sana ya mbinu za wafanyi biashara wakiungana na baadhi ya taasisi za serikali kufanyisha uhaba wa bidhaa flani ili mradi wao wavune mamilioni. Wangelitabiri huu uhaba na kuingiza hayo mahindi ya Mexico miezi mbili tatu mapema. Masilahi ya wanjiku hapa hayana umuhimu. Wameweza kufanya hujuma kama hili na maziwa pia. Pesa linatakikana kwa haraka zaidi, na tusidaganyane hatujui kwa nini. Kwa wale walioishi Kenya hii, mnaweza pia kumbuka ule uhaba wa sukari miaka ya 90 na malengo yake yalikuwa yale yale.
Hata hivyo naomba tule pia mazao mengine. Tuige wenzetu wa afrika magharibi na tule pia yams(hili sijui wanaliitaje kwa kiswahili).
Iconoclastes umetaja zao la yam kama limetokea nje ya afrika lakini sidhani. Limekuwa afrika magharibi enzi na maenzi.