Bulabo ipo chini ya kanisa katoliki wasukuma na wazungu . Wenye tamaasha wameingia mitini
๐ฎ๐ฑ Yes bulabo ni sherehe ya kisukuma iliyochanganywa na sherehe ya kanisa katoliki duniani SIKU KUU YA EKARISTI TAKATIFU. HIii kikanisa ni siku ya mlo ,msosi au bufeee, ndio siku Yesu alipomega mkate na kuwagawia wanafunzi wake wale
๐ฎ๐ฑ Kadhalika kisukuma Bugaboo lilimaanisha sherehe ya baraza la wazee au jando la wanaume hufanyika baada ya mavuno ambapo sherehe za pombe na msosi vikibatana na ulaji wa miwa hufanyika
๐ฎ๐ฑ Kwa kuwa kanisa katoliki na sherehe zilizoambata na Milo iliyoshiba mdudu akiwa sehemu ya kitoweo pamoja na ugimbi au pombe vilipata mwitikio mkubwa miongoni mwa jamii za kisukuma na sherehe hiyo ikawa Moja. Hivyo watasherekea kwa misosi na miwa na baadaye kesho jumapili watafanya ibada ya ekaristi takatifu kwa kuandamana majini na ekaristi
๐ฎ๐ฑ Kanisa katoliki ndio lililokusanya tamaduni za kisukuma na kuanzisha kituo.cha utamaduni ambacho kimekuwa kivutio kikibwa Cha cultural tourism kwa wagenj kutoka nchi mbalimbali duniani kuja kujifunza Mila za kisukuma hasa kutoka nchi za Scandinavia ambao utawakuta kwenye vikundi vya Ngoma vya Bujora na Mwanalyaku wakisakata Bugobogobo na mfano wake ni huyu hapa Manongu,
View: https://youtu.be/Wxp0cDhPtIo?si=AQ8xTPUbGcR3ePZT๐ฎ๐ฑ Tamasha la bulabo la Leo lilikuwa na sura ya kitaifa na kimataifa kwani walimekuja wagenj wengi ambao waliwahi kuishi usukumani ama kwa kuzaliwa au kutembelea na kujifunza Mila na lugha ya kisukuma hufuatilia Kila kinachoendelea na sherehe kama ya Leo ndio wanapata kumbukumbu ya maisha Yao na kuonana na marafiki zao wa utotonj ambao Sasa ni wazee wa kimila
๐ฎ๐ฑ Wagenj wa kiarabu uliowaona Leo ni sehemu ya wazawa wa Tanzania usukumani ambao baba zao walikuwa ni wafanya biashara wa pamba na walizaliwa bongo ,wakasoma bongo na baada ya kurudi kwenye asili Yao bado ule usukuma walioishi haujawaisha
๐ฎ๐ฑ Kadhalika, walikuwepo walikwa machifu kutoka Africa ya kusini na kuleta sura ya ukimataifa
โ๏ธ Hongereni Sana Mwaluko kabudi na mdogo wako Dr. Mapanaa kwa kuipangilia vyema siku hii ya kitamaduni. Naamini Sasa kupitia ninyi vijana wa kigogo ambao utamaduni hauitaji kusomewa mtarejesha heshima ya utamaduni wa nchi ulioharibiwa na dini, mpira wa miguu pamoja na muziki wa bongo flavour
๐น๐ฟ Naamini Sasa ukija ugeni kutoka nje hatuwapokei tena kwa matarumbeta Bali kikundi Cha utamaduni kilichovaa kitamaduni kama Ile minjemba niliyoiona Jana kwenye TV kutoka tabora kwenye Tamasha la sungu sungu kitaifa au yule manju wa Ngoma ya kikerewe niliyoiona live kwenye sherehe ya bulabo ikiwa na vitoto 3 na manju wa kutishana
๐น๐ฟ Nategemea Sasa kupitia sherehii hizi mbili za sungusungu na bulabo wizara imepata au kujua kikundi Cha kusindikiza Timu ya taifa tunapokwrnda kucheza nje ni Cha aina gani na kuachana na wasanii wa majini na wavaa suti. Hivi Tanzania ndio ya kuzidiwa vikundi vya ushangiliaji vya kitamaduni na Zaire? Mwisho wa kunukiu Nakala kwa PROF. KABUDI na DR. MAPANAA aliyeweza kuwaimbisha wazungu nyimbo za kigogo