Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Benjamin William Mkapa akiwa Rais wa Tanzania, aliweka mkazo katika mambo sita (6), yafuatayo;
1. Lengo la demokrasia ni kurejesha nguvu na madaraka kwa wananchi kutoka katika mikono ya watawala..
2. Demokrasia ya uwakilishi inatakiwa kutupatia viongozi wanaoamua kwa niaba yetu na siyo kuamua badala yetu.
3. Tunaowachagua (viongozi wa Serikali kuu na Mitaa) ni watumishi na wawezeshaji wetu na siyo mabwana zetu.
4. Upo umuhimu wa wananchi kujiamimi na kukubali hatima ya kaya, jamii na nchi yetu ipo mikononi kwetu.
5. Serikali inapopeleka madaraka karibu na wananchi inapata ya haki kudai wajibu. Madaraka na wajibu.
6. Demokrasia yetu ijihusishe na vita dhidi ya umaskini, maana penye umaskini demokrasia haiwezi kustawi.