Video: Mdada aenda saluni kusuka wakati hana hela. Alichofanyiwa na mwenye saluni tunaomba Dkt Gwajima aingilie

Video: Mdada aenda saluni kusuka wakati hana hela. Alichofanyiwa na mwenye saluni tunaomba Dkt Gwajima aingilie

Wakuu,

Hivi ni kwamba wanawake hawapendani au imekaaje hii.

Huyu dada alienda saluni, ikatokea tu hana hela wakaamua kwenda kumnyoa na kumrekodi kabisa.

Dkt. Gwajima D tunaomba uitazame hii

View attachment 3250374
Acheni kusumbua watu kwa vitu vidogo. Waziri ana mambo muhimu ya kufanya sio watu kunyoana nywele. Hao wenye wasusi hawana utu kumuachia mtu mmoja inakupunguzia nini? Ningekuwa karibu hapo ningemlipia huyo dada.
 
Asichukie, aendelee kunyoa tu bado atapendeza.

Huyu nae,aliendaje saloon bila hela..anadhani kazi nyepesi hiyo,?🤔

Hao nao,Nini kumnyoa mwenzao...si wangemwambie afumue tu mwenyewe kabla hawajamfanyia umafia🙄

Angefumua mwenyewe hasingepata fundisho.

Ndio maana makosa yakawekewa adhabu.

Kunyolewa ndio adhabu yake
 
Wanawake tunapenda mambo makubwa mambo makuu Ili kufanya show off Kwa watu ama shoga zako tuishi Kwa kipato chetu jaman tuache kutumia nguvu kubwa kias icho mpaka udhalilike Nina shuhuda nyingi sana kuhusu hii hatukomi tubadilike watoto wakike ni aibuu.

Tufanye kazi tujitoe kwenye aibu kama hii
 
Acheni kusumbua watu kwa vitu vidogo. Waziri ana mambo muhimu ya kufanya sio watu kunyoana nywele. Hao wenye wasusi hawana utu kumuachia mtu mmoja inakupunguzia nini? Ningekuwa karibu hapo ningemlipia huyo dada.

Ukimuachia mtu bila adhabu unakuwa hujamfundisha.

Huyo amepewa adhabu nzuri ya kuacha kuchezea biashara za watu.

Siku nyingine hatarudia tena hilo kosa
 
Ukimuachia mtu bila adhabu unakuwa hujamfundisha.

Huyo amepewa adhabu nzuri ya kuacha kuchezea biashara za watu.

Siku nyingine hatarudia tena hilo kosa
Unamuchia huku ukimpa onyo na funzo, wewe utalipwa na Mungu. Hasara roho pesa makaratasi.
 
Unamuchia huku ukimpa onyo na funzo, wewe uta;ipwa na Mungu. Hasara roho pesa makaratasi.

Serikali yenyewe haisamehi makosa. Ndio maana tusipolipa bill tunakatiwa maji na inaongezeka faini juu, kwenye kosa la barabarani traffic wanatupiga fine..

Bila kumpa adhabu binadamu ataleta mchezo sana
 
Huyu dada hajafanya vizuri. Huo ni uhalifu. Ila wenye saluni nao ni wapumbavu kwa kuchafua brand yao kipuuuzi. Wateja wataiogopa hiyo saluni.
 
Unamuchia huku ukimpa onyo na funzo, wewe utalipwa na Mungu. Hasara roho pesa makaratasi.
Kuna misuko watu wanatumia masaa zaidi ya manne tena wapo wawili, kwa msusi hiyo ni hasara kubwa ya muda wake.
Nadhani anastahili adhabu, huenda hiyo imekuwa kali kidogo ila kwa vile nywele zinaota tu, hakuna shida, atajifunza na ni funzo kwa wengine pia.
 
Back
Top Bottom