DOKEZO Video: Mdada wa Kinondoni aliyeenda kufanya kazi za ndani Iraq afichiwa passport na mwajiriwa wake. Anyimwa chakula na kupitia mateso

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wakati mwingine ni ngumu kuwaelewa Watanzania.... Mwaka 2022 kuna binti anafahamiana na mdogo wangu wa kike, siku moja kama home, anamwambia mdogo wangu maisha ya Tanzania yamemshinda anaenda Iraq kufanya kazi!

Nikajaribu kuongea nae, huko kuna slavery , sio kazi za kawaida! Akakaza shingo, baada ya kama wiki naambiwa kaacha mizigo yake home, safari Iraq. Baada ya mwezi tu, kaanza kumsumbua mdogo wangu, anataka kurudi home sijui kalikwenda kakarudi. Boss kamwambia, kama unataka kurudi kwanza ulipe gharama, usd 6,000 anazitoa wapi! Ndugu zake hoe hae.

Watu wa Arab countries kwa ujumla wanamuona mtu mweusi kuwa sio binadamu! Ni bora ukutane na mzungu wa hovyo kabisa kuliko watu wa Arab countries. Wapo waliorushwa ghorofani wakafa, wapo waliofanyishwa mapenzi na mbwa.
 
Wakuu,

Mtanzania mwenye umri wa miaka 33, Fatma Nassoro anapitia mateso makubwa akiwa nchini Iraq, ambako alienda kufanya kazi tangu mwaka 2022. Fatma amesema amekuwa akiishi katika mazingira magumu chini ya mwajiri wake, huku akinyimwa chakula, kupigwa mara kwa mara, kutukanwa, kubezwa, na hata kutemewa mate.

Juhudi zake za kutaka kurejea nyumbani zimegonga mwamba baada ya mwajiri wake kuficha pasipoti yake, akimzuia kuondoka. Mwaka jana, Fatma alipata msiba mzito baada ya kufiwa na mtoto wake, lakini alinyimwa ruhusa ya kurudi Tanzania kuhudhuria mazishi.

Kwa sasa, hali imezidi kuwa ngumu, huku afya ya mama yake ikiwa dhoofu, lakini bado ameshindwa kurudi kumwona. Fatma anasema Iraq haina ubalozi wa Tanzania, hali iliyomwacha bila msaada wa karibu wa kisheria au ulinzi.

Amebainisha kuwa anawasiliana kwa siri kupitia namba ya jirani wakati mwajiri wake hayupo, akitafuta msaada wa kurejea nyumbani. Fatma anatoa wito kwa mamlaka za Tanzania na mashirika ya haki za binadamu kumsaidia kurejea salama na kumaliza mateso anayopitia.

huyu atakuwa amepeleka uswahili kwenye kazi za watu (ubishi na ujuaji) ndio wameamua kumnyoosha sasa anaanza kusumbua watu!
 
Waarabu hata wa kwetu Tanzania ni wabaguzi sn... kwanza ni vigumu sana kumkuta binti wa kiarabu ameolewa na ngozi nyeusi ila ni rahisi mno mwafrika kumuoa Mzungu... Popote walipo Waarabu sio watu Wazuri...
 
Acha chuki na wale wanaoteswa hapa hapa bongo na wakinamama waliokosa malezi hao ni waarabu nao.
Huyo bahati mbaya tu kaangukia kwenye sufuria la uji.
Tabia hazina uhusiano na race
Lakini uarabuni wamezidi hata walioenda wakirudi huwa hawatamani tena kurudi kule
 
Sasa unalia nini? hizo ndio ajira mlizotafutiwa na mama yenu kigulu na njia mnaedai anaupiga mwingi
Huyu mwajiri mbona malaika je ungekutana na Chemical Ali?
 
Najua inaweza isilipe kisiasa ila kibinadamu ni mzuri, viongozi wamsaidie huyo binti. Najua hamshindwi kimsusa tu.
 
Wakuu,

Mtanzania mwenye umri wa miaka 33, Fatma Nassoro anapitia mateso makubwa akiwa nchini Iraq, ambako alienda kufanya kazi tangu mwaka 2022. Fatma amesema amekuwa akiishi katika mazingira magumu chini ya mwajiri wake, huku akinyimwa chakula, kupigwa mara kwa mara, kutukanwa, kubezwa, na hata kutemewa mate.

Juhudi zake za kutaka kurejea nyumbani zimegonga mwamba baada ya mwajiri wake kuficha pasipoti yake, akimzuia kuondoka. Mwaka jana, Fatma alipata msiba mzito baada ya kufiwa na mtoto wake, lakini alinyimwa ruhusa ya kurudi Tanzania kuhudhuria mazishi.

Kwa sasa, hali imezidi kuwa ngumu, huku afya ya mama yake ikiwa dhoofu, lakini bado ameshindwa kurudi kumwona. Fatma anasema Iraq haina ubalozi wa Tanzania, hali iliyomwacha bila msaada wa karibu wa kisheria au ulinzi.

Amebainisha kuwa anawasiliana kwa siri kupitia namba ya jirani wakati mwajiri wake hayupo, akitafuta msaada wa kurejea nyumbani. Fatma anatoa wito kwa mamlaka za Tanzania na mashirika ya haki za binadamu kumsaidia kurejea salama na kumaliza mateso anayopitia.

Nchi za kiislamu zote siyo za kuishi. Ukiwaambia watu wanasema ni ndugu zao
Apambane nao
 
Duh! watu wanafika hadi Iraq?

Kuna kile kitengo cha UN kinaitwa IMO kama sikosei, kipo karibu kila nchi, huwa pia wanasafiriaha raia kurudi katika mataifa yao.

Angeweza kufika katika ofisi zao angepata msaada.
IOM
 
Wakuu,

Mtanzania mwenye umri wa miaka 33, Fatma Nassoro anapitia mateso makubwa akiwa nchini Iraq, ambako alienda kufanya kazi tangu mwaka 2022. Fatma amesema amekuwa akiishi katika mazingira magumu chini ya mwajiri wake, huku akinyimwa chakula, kupigwa mara kwa mara, kutukanwa, kubezwa, na hata kutemewa mate.

Juhudi zake za kutaka kurejea nyumbani zimegonga mwamba baada ya mwajiri wake kuficha pasipoti yake, akimzuia kuondoka. Mwaka jana, Fatma alipata msiba mzito baada ya kufiwa na mtoto wake, lakini alinyimwa ruhusa ya kurudi Tanzania kuhudhuria mazishi.

Kwa sasa, hali imezidi kuwa ngumu, huku afya ya mama yake ikiwa dhoofu, lakini bado ameshindwa kurudi kumwona. Fatma anasema Iraq haina ubalozi wa Tanzania, hali iliyomwacha bila msaada wa karibu wa kisheria au ulinzi.

Amebainisha kuwa anawasiliana kwa siri kupitia namba ya jirani wakati mwajiri wake hayupo, akitafuta msaada wa kurejea nyumbani. Fatma anatoa wito kwa mamlaka za Tanzania na mashirika ya haki za binadamu kumsaidia kurejea salama na kumaliza mateso anayopitia.

Yaani utoke Tanzania ukafanye kazi Iraq,Iran, Afghanistan?
Kazi Gani hiyo yenye thamani wakupe ambayo huo mshahara bongo haupo?
 
Back
Top Bottom