DOKEZO Video: Mdada wa Kinondoni aliyeenda kufanya kazi za ndani Iraq afichiwa passport na mwajiriwa wake. Anyimwa chakula na kupitia mateso

DOKEZO Video: Mdada wa Kinondoni aliyeenda kufanya kazi za ndani Iraq afichiwa passport na mwajiriwa wake. Anyimwa chakula na kupitia mateso

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
"Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, na kufanya wema, na kuwapa jamaa (haki zao), na anakataza machafu, na munkari, na dhuluma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka."
— Qur'an 16:90
Unashabikia CCM!
 
Hawa watu bado waamini mtumishi wao ni mtumwa tu, ukiwa mweusi ndio kabisaa inakuwa issue.

Kuna ubalozi wa Tanzania hapo Kuwait, watumiwe hiyo clip wawasiliane na Serikali ya Iraq taratibu nyingine zifanyike.

Umasikini ni kitu kibaya sana.
 
Magu alipiga pin hakuna visa ya kwenda kufanya hizi kazi mpaka uwe na mkataba wa kueleweka wakamwona mbaya.
 
📌📌📌Alienda kimya kimya huko Uarabuni tena ukute alitoa na hongo ili apate kipaumbele🤗 basi na arudi kimyakimya.Hatutaki kelele tunamambo mengi ya kufanya🤝
 
Hatuna ubalozi Iraq, lakini anaweza kupata msaada toka ubalozi wa Uingereza. Maadam yeye ni Mwananchi wa Tanzania ambayo ni Nchi mwanachama wa Commonwealth na UK ndiye Kiranja wake, ni rahisi kupata msaada. Ushahidi upo watu wamesaidiwa kurudi Tanzania kupitia UK Embassy.

Achukue ushauri huu kama kweli anataka kirudi nchi ya CCm.
 
Mshahara wa dada wa KAZI hata mwenye elimu ya Masters bongo apati.
Mengine ni ajali kazini
Mkienda na hizi mentality kwasababu ya kukimbia umande.Yakiwakuta majambo msianze kurusha viclip kutaka huruma.

📌📌📌Mmechagua kuhustle then go f*ckn hustle like shit!!!
 
Wakati mwingine ni ngumu kuwaelewa Watanzania.... Mwaka 2022 kuna binti anafahamiana na mdogo wangu wa kike, siku moja kama home, anamwambia mdogo wangu maisha ya Tanzania yamemshinda anaenda Iraq kufanya kazi!

Nikajaribu kuongea nae, huko kuna slavery , sio kazi za kawaida! Akakaza shingo, baada ya kama wiki naambiwa kaacha mizigo yake home, safari Iraq. Baada ya mwezi tu, kaanza kumsumbua mdogo wangu, anataka kurudi home sijui kalikwenda kakarudi. Boss kamwambia, kama unataka kurudi kwanza ulipe gharama, usd 6,000 anazitoa wapi! Ndugu zake hoe hae.

Watu wa Arab countries kwa ujumla wanamuona mtu mweusi kuwa sio binadamu! Ni bora ukutane na mzungu wa hovyo kabisa kuliko watu wa Arab countries. Wapo waliorushwa ghorofani wakafa, wapo waliofanyishwa mapenzi na mbwa.
Ukiachana na arab slave mind watanzania. sio wachapakazi ni majitu mavivu na malalamishi.

Watanzania mda wote wanawaza kutoboa kwa zali.Hawaamini katika kuteseka kupata mafanikio.

Huyo rafiki wa ndugu yako alizani kwenda Iraq ni kwenda Kkoo😀😀😀.

📌📌📌Kama mtu ameshindwa kujimake katika hii nchi isiyo na mifumo imara na iliyo na kila kitu chances za kujimake nchi za watu zilizo na mifumo ni ngumu sana.
 
Wakuu,

Mtanzania mwenye umri wa miaka 33, Fatma Nassoro anapitia mateso makubwa akiwa nchini Iraq, ambako alienda kufanya kazi tangu mwaka 2022. Fatma amesema amekuwa akiishi katika mazingira magumu chini ya mwajiri wake, huku akinyimwa chakula, kupigwa mara kwa mara, kutukanwa, kubezwa, na hata kutemewa mate.

Juhudi zake za kutaka kurejea nyumbani zimegonga mwamba baada ya mwajiri wake kuficha pasipoti yake, akimzuia kuondoka. Mwaka jana, Fatma alipata msiba mzito baada ya kufiwa na mtoto wake, lakini alinyimwa ruhusa ya kurudi Tanzania kuhudhuria mazishi.

Kwa sasa, hali imezidi kuwa ngumu, huku afya ya mama yake ikiwa dhoofu, lakini bado ameshindwa kurudi kumwona. Fatma anasema Iraq haina ubalozi wa Tanzania, hali iliyomwacha bila msaada wa karibu wa kisheria au ulinzi.

Amebainisha kuwa anawasiliana kwa siri kupitia namba ya jirani wakati mwajiri wake hayupo, akitafuta msaada wa kurejea nyumbani. Fatma anatoa wito kwa mamlaka za Tanzania na mashirika ya haki za binadamu kumsaidia kurejea salama na kumaliza mateso anayopitia.

Dini ya haki inamuona Mwarabu NDIYE kiumbe pekee wa mola, nyie wengine simbilisi tu
 
Yaani utoke Tanzania ukafanye kazi Iraq,Iran, Afghanistan?
Kazi Gani hiyo yenye thamani wakupe ambayo huo mshahara bongo haupo?
📌📌📌Ni upotevu wa muda na kundi danganyika ni wale wanzangu na mie waliokimbia UMANDE!!!
 
Anaitwa fatma ina maana hao ndi ndugu zake katika imaan

Lakini bado wanamnyanyasa, mkiambiwa hiyo dini ya kuvaa kobazi ni empty set na vurugu hamtaki kuelewa
📌📌Dini zote ni UJINGA na tool ya kuwafanya watu wawe watii.
 
Wakuu,

Mtanzania mwenye umri wa miaka 33, Fatma Nassoro anapitia mateso makubwa akiwa nchini Iraq, ambako alienda kufanya kazi tangu mwaka 2022. Fatma amesema amekuwa akiishi katika mazingira magumu chini ya mwajiri wake, huku akinyimwa chakula, kupigwa mara kwa mara, kutukanwa, kubezwa, na hata kutemewa mate.

Juhudi zake za kutaka kurejea nyumbani zimegonga mwamba baada ya mwajiri wake kuficha pasipoti yake, akimzuia kuondoka. Mwaka jana, Fatma alipata msiba mzito baada ya kufiwa na mtoto wake, lakini alinyimwa ruhusa ya kurudi Tanzania kuhudhuria mazishi.

Kwa sasa, hali imezidi kuwa ngumu, huku afya ya mama yake ikiwa dhoofu, lakini bado ameshindwa kurudi kumwona. Fatma anasema Iraq haina ubalozi wa Tanzania, hali iliyomwacha bila msaada wa karibu wa kisheria au ulinzi.

Amebainisha kuwa anawasiliana kwa siri kupitia namba ya jirani wakati mwajiri wake hayupo, akitafuta msaada wa kurejea nyumbani. Fatma anatoa wito kwa mamlaka za Tanzania na mashirika ya haki za binadamu kumsaidia kurejea salama na kumaliza mateso anayopitia.

As long as muslims to muslims we dont care
 
Back
Top Bottom