DOKEZO Video: Mdada wa Kinondoni aliyeenda kufanya kazi za ndani Iraq afichiwa passport na mwajiriwa wake. Anyimwa chakula na kupitia mateso

DOKEZO Video: Mdada wa Kinondoni aliyeenda kufanya kazi za ndani Iraq afichiwa passport na mwajiriwa wake. Anyimwa chakula na kupitia mateso

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kujikuta matatani kwa wadada wa kazi inaweza kutokea hata ndani ya nchi Cha msingi wahanga kutafuta mbinu ya kufikisha taarifa kuomba msaada, maisha popote.
Nenda VETA mkasome fani mpate ujuzi mjitegemee na kujitetea ,muache kupenda vya mserereko hakuna cha ndugu katika imani wala ushubwada wa namna hiyo.

📌📌Himizeni watoto wasome fani wapate ujuzi.Itawasaidia kujitafutia maisha.Kazi za ndani hazijawahi kumtoa mtu kimaisha zaidi ya vilio tu tena ukute jitu ni vivu🤗🤗🤗🤗
 
Wapo waliojenga majumba ya kifahari,wapo walionunulia wazazi wao majumba.Wapo waliopata mitaji ya biashara.
Amefanya kazi za ndani miaka mingapi mpaka kujenga nyumba ya maana( majumba)😂😂😂

Wabongo hizi stori za vijiwe vya kahawa migomigo,kino na ilala bwana.Hao punda wa ngada ndio wanafanya hivyo vitu mnaita maendeleo ila kwa kazi za ndani labda mtu afanye kwaanzia miaka 20 plus.
 
Waarabu wana roho mbaya, tatizo watu wakiambiwa hawaelewi..!!
 
Hapo ndio kwenye shida, kazi ya house girl ukishareport kazini kurudi ni baada ya mwaka au miaka miwili ndio unapewa ticket ya safai. sasa ukianza uswahili ya ooh Mama anaumwa au naomba ruhusa nimefiwa shida ndio zinaanzia hapo
Mibongo ni mivivu hizo kazi haiwezi kufanya ila ushamba wa kusafiri na kupanda ndege ndio umewajaa wakishafika huko uarabuni akili ndo zinarudi anaona bora Bongoland ugali na uono na maziwa mtindi maisha swaafi kabisa😀😀😀
 
Kila siku mnaambiwa waarabu sio watu hamuelewi...akome
Ila ujue waKenya wapo huko kwa maeLfu na ni moja ya source ya kuipatia Nchi yao hela za kigeni;
Sikatai kuwa kuna watu wachache wanateseka ambapo ni jambo baya hata kama ni 1% lakini ujue tu sio Waarabu wote wabaya. Umefika DXB Airport siku za karibuni? niliona ni wakenya wamejaa huko karibia kila Idara ndio wanahudumia watu...pengine lugha inawabeba!
Nafikiri na sisi tubadilike tulenge kupeleka wafanyakazi na sio vibarua wa kazi za ndani.....
Hivi unafikiri Nchi nyingine waafrika wasio na elimu ya kueleweka hawanyanyaswi? Tembea uone!
 
But penye wabaya wema nao wapo.
Na hao wa dada waliobadilisha maisha ya familia zao bongo mwaka wa kumi sasa wapo wanapiga kazi huko je hawa wameteswa na nani.
Pana mpaka waliolewa huko
📌📌Acheni kujifariji kufanya kazi za ndani sio kazi.Himizeni watoto kusoma na kufaulu au kwenda VETA kujipatia ujuzi na fani kuliko kupigia chapuo huu UTUMWA!!!
 
Ila ujue waKenya wapo huko kwa maeLfu na ni moja ya source ya kuipatia Nchi yao hela za kigeni;
Sikatai kuwa kuna watu wanateseka ambapo ni jambo baya sana (hatakama ni 1%) lakini ujue tu sio waarabu wote wabaya. Umefika DXB Airport siku za karibuni? niliona ni wakenya wamejaa huko karibia kila Idara ndio wanahudumia watu...pengine lugha inawabeba!
Nafikiri na sisi tubadilike tulenge kupeleka wafanyakazi na sio vibarua wa kazi za ndani.....
Yaani kisa wakenya wamefanya na nyie mfanye hivi nyie watu mlienda shule kweli???

Kama shule ilikuwa ngumu kwanini msiende shamba mkalime🤔
 
Hakuna cha uswahili hapo, nenda wewe basi kawaoneshe uzungu wako na ngozi yako nyeusi kama hawajakutumbukiza kwenye shimo la taka
suala ni kwanini akafanye kazi za ndani ughaibuni wakati kazi hizo hata hapa nyumbani zipo! Ingekuwa kazi ya kisomo ujinga huo usingekuwepo,hivyo ni afadhali angeenda shamba akalime na angekuwa na vyake na amani tele kuliko huo ujinga wanaofanyiwa huko!
 
Yaani kisa wakenya wamefanya na nyie mfanye hivi nyie watu mlienda shule kweli???

Kama shule ilikuwa ngumu kwanini msiende shamba mkalime🤔

Dunia imeshafika "AI" bosi, huwezi kuishi Nchini kwako kama kijiji
Hata hivyo wakenya wapo mbali.... tusijidanganye. Kama kuna mambo mazuri kwao, ni vizuri tuige.
Narudia tena; tunatakiwa tupeleke WAFANYAKAZI na sio vibarua wa kazi za ndani!
 
Dunia imeshafika "AI" bosi, huwezi kuishi Nchini kwako kama kijiji
Hata hivyo wakenya wapo mbali.... tusijidanganye. Kama kuna mambo mazuri kwao, ni vizuri tuige.
Narudia tena; tunatakiwa tupeleke wafanyakazi na sio vibarua wa kazi za ndani!
Narudia msiwapeleke wenzenu wasio na ufahamu utumwani.

Dunia kijiji ila sio kwa masikini kama Tz.
 
Wakuu,

Mtanzania mwenye umri wa miaka 33, Fatma Nassoro anapitia mateso makubwa akiwa nchini Iraq, ambako alienda kufanya kazi tangu mwaka 2022. Fatma amesema amekuwa akiishi katika mazingira magumu chini ya mwajiri wake, huku akinyimwa chakula, kupigwa mara kwa mara, kutukanwa, kubezwa, na hata kutemewa mate.

Juhudi zake za kutaka kurejea nyumbani zimegonga mwamba baada ya mwajiri wake kuficha pasipoti yake, akimzuia kuondoka. Mwaka jana, Fatma alipata msiba mzito baada ya kufiwa na mtoto wake, lakini alinyimwa ruhusa ya kurudi Tanzania kuhudhuria mazishi.

Kwa sasa, hali imezidi kuwa ngumu, huku afya ya mama yake ikiwa dhoofu, lakini bado ameshindwa kurudi kumwona. Fatma anasema Iraq haina ubalozi wa Tanzania, hali iliyomwacha bila msaada wa karibu wa kisheria au ulinzi.

Amebainisha kuwa anawasiliana kwa siri kupitia namba ya jirani wakati mwajiri wake hayupo, akitafuta msaada wa kurejea nyumbani. Fatma anatoa wito kwa mamlaka za Tanzania na mashirika ya haki za binadamu kumsaidia kurejea salama na kumaliza mateso anayopitia.

Hawa c ndo kutwa kucha wanawasifia waarabu na kuwapondea wazungu kwamba ni mabeberu yanatutesa acha ale Malipo yake
 
Hawa nao hawasikiagi acha wateseke,kila kukicha watu wanasema sio mtaani wala mitandaoni,hao watu ni dogii kama dogii wengine na nyie mnaenda kukaa nao
Alafu mbona kama analia uongo
 
Ila hawa watu nao jamani khaaa,. Tangu niko mdogo nasikiaga tu wakilalamika hivihivi sijui kwanini hawajifunzi kwa wenzao.. Kwani kazi sehemu nyingine zenye usalama hakuna ??
Shida kupanda ndege..
 
Nenda VETA mkasome fani mpate ujuzi mjitegemee na kujitetea ,muache kupenda vya mserereko hakuna cha ndugu katika imani wala ushubwada wa namna hiyo.

📌📌Himizeni watoto wasome fani wapate ujuzi.Itawasaidia kujitafutia maisha.Kazi za ndani hazijawahi kumtoa mtu kimaisha zaidi ya vilio tu tena ukute jitu ni vivu🤗🤗🤗🤗
Hata wasomi walioajiriwa na mashirika ya kimataifa katika nchi za kigeni hukumbwa na misukosuko, hata wote tukisoma maids watahitajika tu Cha msingi ni maslahi.
 
Hata wasomi walioajiriwa na mashirika ya kimataifa katika nchi za kigeni hukumbwa na misukosuko, hata wote tukisoma maids watahitajika tu Cha msingi ni maslahi.
Sawa endeleeni kufanya kazi za kijungu jiko!!!
 
Ila ujue waKenya wapo huko kwa maeLfu na ni moja ya source ya kuipatia Nchi yao hela za kigeni;
Sikatai kuwa kuna watu wanateseka ambapo ni jambo baya sana (hatakama ni 1%) lakini ujue tu sio waarabu wote wabaya. Umefika DXB Airport siku za karibuni? niliona ni wakenya wamejaa huko karibia kila Idara ndio wanahudumia watu...pengine lugha inawabeba!
Nafikiri na sisi tubadilike tulenge kupeleka wafanyakazi na sio vibarua wa kazi za ndani.....

hata hao wakenya mkuu wapo kwenye kila sector, hata hizo house maid wamejaa. na Tatizo ni jamaa zetu wa TZ wana very nagative minds, na ndio mana sisi tutendelea kuwa nyuma tu.ukienda nchi za kiarabu ukaona watu wa mataifa mengine ya kiafrica wanavyokula maisha huwa inauma sana
 
Back
Top Bottom