SI KWELI Video: Miamba imeporomoka watu wakiwa wanapanda

SI KWELI Video: Miamba imeporomoka watu wakiwa wanapanda

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na kipande cha video kikionesha wanaoonekana watalii wakipanda miamba na kishawanadondokewa na miamba hiyo ni halisi?


Screenshot 2025-06-23 091558.png
 
Tunachokijua
Madai

Kumekuwepo kipande cha video kinachowaonesha watu wanaoonekana kama watalii wakipanda miamba wanaporomokewa na miamba hiyo muda mfupi tu wakiwa wanapanda. Kipande hiko kimesambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo instagram.

Uhalisia wa video hiyo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa kipande hiko cha video si halisi bali kimetengenezwa kwa teknolojia ya akili unde (AI). Kwa kutumia Video reverse search Ufuatiliaji umebaini video hiyo ina matendo ambayo si ya kawaida.

Miongoni mwa matukio yasiyo ya kawaida katika video hiyo ni linalonesha wakati watu wengine wakionekana kudondokewa na miamba hiyo, wapandaji wengine hawaonekani kushtushwa na wanaendelea na zoezi la upandaji bila wasiwasi.

Watu wanaonekana kwenye video hiyo hawana maumbo kamili mathalani mikono yao hainokeani kuwa imeshika kitu pia wana mwendo usio wa kawaida. Aidha wanaonekana wakiyeyuka na kuwa na maumbo yasiyo ya kawaida mara baada ya kudondekewa na miamba hiyo

Aidha Sauti inayosikika nyuma ya video hiyo haiendani na matukio yanayooneakana hivyo kupoteza uhalisia wa video hiyo. Mathalani sauti ya kishindo kinachoashiria kudondoka kwa mlima ama miamba hiyo inapishana na kinachoonekana. Vile vile sauti ya wanaopiga kelele hainokeani kuwa halisi.

Mwishoni mwa video hiyo unaonekana mti ambao haunokeani kuwa umetikiswa kwa namna yoyote ile, aidha mti huo unaonekana kuwa uliota ndani ya miamba hiyo jambo ambalo si halisi.
AI video
Jiulize hiyo miti imetokea wapi baada ya miamba kuporomoka
 
Back
Top Bottom