Media yakenya inavyo wakuza,hawa du!!!
Sauti Sol wazindua video ya ngoma 'Kuliko Jana'
Imepakiwa - Tuesday, September 13 2016 at 10:19
MAJAGINA wa muziki wa Afrika Mashariki na washindi wa tuzo kibao, Sauti Sol (Kenya) wameachia video ya wimbo wao unaofanya vizuri, Kuliko Jana, uliopo kwenye albamu yao ya tatu: Live and Die in Afrika iliyozinduliwa rasmi Februari 2016.
Bien wa Sauti Sol anaelezea maana ya wimbo huo, “Unamaanisha kuwa uaminifu wa Mungu haukomi kamwe.
Huruma yake haiishi – kila uchao ni vipya.”
Wakimshirikisha Redfourth Chorus (Upper Hill School), wimbo huo mtamu lakini wenye ujumbe mzito, umeendelea kupanda chati na kuwagusa mashabiki barani Afrika na zaidi.
Katika video mpya iliyotoka yenye rangi nyeusi na nyeupe ya Kuliko Jana, Sauti Sol wameungana na chipukizi lakini mwenye kipawa cha hali ya juu, Redfourth Chorus kwa maajabu ya kimuziki.
Sauti Sol wamesema kwenye taarifa yao, “Kuliko Jana ni wimbo maalum sana kwetu. Ulihamasishwa na safari yetu na rehema zisizoisha, mapenzi na baraka ambazo Mungu ametuonesha muda wote licha ya udhaifu wetu.”
Video ya Kuliko Jana imetayarishwa na Fulfillment Limited, na kufanyika Kenya na waongozaji wakiwa Tim Mwaura na Joash Omondi.
Wimbo umeandikwa na kutayarishwa na Sauti Sol.
Kipande cha akapela kilipangwa na Philip Tuju na Redfourth Chorus.