Video mpya: Sauti Sol - Kuliko Jana!

Video mpya: Sauti Sol - Kuliko Jana!

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2016
Posts
10,518
Reaction score
13,144
1473746079764.jpg
Kwa wale wapenda mziki mzuri Sauti sol wameachia video ya wimbo wao unaoitwa kuliko Jana,ngoma iko poa sana na video yake iko poa unaweza kuitazama hapo chini nimeiweka!
 
Yesu ni mwokozi wangu, tena ni kiongozi wangu, ananipenda leo kuliko jana. Baraka zake hazikwishi si kama binadamu habadiliki. Ananipenda leo kuliko jana. Kuliko jana, kuliko jana, Yesu nipende leo kuliko jana.

Haki vile vijana wanaimba hawabahatisha
 
Media yakenya inavyo wakuza,hawa du!!!

Sauti Sol wazindua video ya ngoma 'Kuliko Jana'

Imepakiwa - Tuesday, September 13 2016 at 10:19



MAJAGINA wa muziki wa Afrika Mashariki na washindi wa tuzo kibao, Sauti Sol (Kenya) wameachia video ya wimbo wao unaofanya vizuri, Kuliko Jana, uliopo kwenye albamu yao ya tatu: Live and Die in Afrika iliyozinduliwa rasmi Februari 2016.

Bien wa Sauti Sol anaelezea maana ya wimbo huo, “Unamaanisha kuwa uaminifu wa Mungu haukomi kamwe.

Huruma yake haiishi – kila uchao ni vipya.”
Wakimshirikisha Redfourth Chorus (Upper Hill School), wimbo huo mtamu lakini wenye ujumbe mzito, umeendelea kupanda chati na kuwagusa mashabiki barani Afrika na zaidi.

Katika video mpya iliyotoka yenye rangi nyeusi na nyeupe ya Kuliko Jana, Sauti Sol wameungana na chipukizi lakini mwenye kipawa cha hali ya juu, Redfourth Chorus kwa maajabu ya kimuziki.

Sauti Sol wamesema kwenye taarifa yao, “Kuliko Jana ni wimbo maalum sana kwetu. Ulihamasishwa na safari yetu na rehema zisizoisha, mapenzi na baraka ambazo Mungu ametuonesha muda wote licha ya udhaifu wetu.”

Video ya Kuliko Jana imetayarishwa na Fulfillment Limited, na kufanyika Kenya na waongozaji wakiwa Tim Mwaura na Joash Omondi.

Wimbo umeandikwa na kutayarishwa na Sauti Sol.
Kipande cha akapela kilipangwa na Philip Tuju na Redfourth Chorus.
 
Back
Top Bottom