Video mpya: Sauti Sol - Kuliko Jana!

Video mpya: Sauti Sol - Kuliko Jana!

Media yakenya inavyo wakuza,hawa du!!!

Sauti Sol wazindua video ya ngoma 'Kuliko Jana'

Imepakiwa - Tuesday, September 13 2016 at 10:19

MAJAGINA wa muziki wa Afrika Mashariki na washindi wa tuzo kibao, Sauti Sol (Kenya) wameachia video ya wimbo wao unaofanya vizuri, Kuliko Jana, uliopo kwenye albamu yao ya tatu: Live and Die in Afrika iliyozinduliwa rasmi Februari 2016.

Bien wa Sauti Sol anaelezea maana ya wimbo huo, “Unamaanisha kuwa uaminifu wa Mungu haukomi kamwe.

Huruma yake haiishi – kila uchao ni vipya.”
Wakimshirikisha Redfourth Chorus (Upper Hill School), wimbo huo mtamu lakini wenye ujumbe mzito, umeendelea kupanda chati na kuwagusa mashabiki barani Afrika na zaidi.

Katika video mpya iliyotoka yenye rangi nyeusi na nyeupe ya Kuliko Jana, Sauti Sol wameungana na chipukizi lakini mwenye kipawa cha hali ya juu, Redfourth Chorus kwa maajabu ya kimuziki.

Sauti Sol wamesema kwenye taarifa yao, “Kuliko Jana ni wimbo maalum sana kwetu. Ulihamasishwa na safari yetu na rehema zisizoisha, mapenzi na baraka ambazo Mungu ametuonesha muda wote licha ya udhaifu wetu.”

Video ya Kuliko Jana imetayarishwa na Fulfillment Limited, na kufanyika Kenya na waongozaji wakiwa Tim Mwaura na Joash Omondi.

Wimbo umeandikwa na kutayarishwa na Sauti Sol.
Kipande cha akapela kilipangwa na Philip Tuju na Redfourth Chorus.
I think bdo wangewakuza hata zaid..hakuna band bora EA kama Sauti Soul, Yamoto hawaingii hata nusu
 
acha wivu kakaaa....!!

wanajuaaaaaaa...!!

kibongo bongo hapa tutasubiri sana tu!
 
Sikilizeni vocal za hatari, sio wabongo flavian wetu wanao imba flat, hawa jamaa wapo vizuri, yaani naamini hata umeme usipokuwepo wanapiga shoo kama kawaida

Nabii hakubaliki kwao mkuu, hebu angalia Diamond anavyojaza kumbi za huko kwao! Wakati huo huo sisi kila siku tunamponda
 
Hao jamaa wanajua sana,lakini hawatii maguu kwa Ya Moto band. Ngoja nisubiri mapovu.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]oy kifesi acha utani usiwafananishe kabisa hao sauti sol ni habari nyingine kabisa jaribu kupita huko youtube kwenye page yao uwone balaa lao!
 
Raimundo sikia, diamond platnumz anapondwa na wajinga wenye chuki ambao hawajui sababu gani wanamchukia diamond platnumz na inakuzwa tu, lkn hamna msanii anayependwa kama diamond platnumz kuanzia tz mpaka EA (endorsement alizokuwanazo zinaprove nguvu yake) na ndio maana MAPARASITE kutwa wanataka kujiattach kwake kwa kutengeneza beef, ila sauti sol ni watu wengine kabisa, ila sijajua kwa nn jamaa hawa kwao nao wanapondwa.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]oy kifesi acha utani usiwafananishe kabisa hao sauti sol ni habari nyingine kabisa jaribu kupita huko youtube kwenye page yao uwone balaa lao!
Kuna balaa gani mkuu .....?
 
Nenda ukaone kazi zao kuna video zao na show zao walizofanya alafu uje utuletee maelezo unaweza kuwafananisha na hao uliowataja!
Basi poa,ila mimi kwa maono yangu Ya Moto band wako juu.
 
Back
Top Bottom