VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

Nina wasiwasi kama hiyo Jumatatu wataongea hawa na kama wataongea je, watakuwa tayari kusema ukweli kuhusu yaliyowakuta kuanzia walipotekwa mpaka walipoachiwa hiyo saa tisa za usiku. Ni akina nani waliowateka? Waliwapeleka wapi? sababu za kuwateka ni zipi? Na kwanini walichukua TV, camera na vifaa vyao vingine toka studio? Je vifaa vyao vimerudishwa vikiwa salama? Inasemekana mmoja wao message zake za whatsapp zilikuwa zinasomwa je, ni mhusika ndiye aliyekuwa anazisoma au wahuni waliowateka?

Movie inatengenezwa na wamepewa warning wasiongee chochote sasa hivi mpaka watakapolishwa maneno.
 
Dah! Wewe ni mzuri wa kusoma watu. Mie pia nimeona hilo la uso wake kuonyesha hofu kubwa. Ngoja tusubiri hiyi Jumatatu kama ataweza kufunguka na kusema kila kitu kilichojiri lakini kwa Serikali hii dhalimu wanaweza kupewa vitisho vya kufa mtu wasiseme chochote kilichojiri.
What the regional government is doing to these kids ain't right at all!!! I hope kunasiku wataumbuka oppenly kabisaaaaa!!! This is murder!!!! and the master mind of all these issues is there pretending to help!!! Kweli TU wajinga nimelia kiukweli!!! Kijana wawatu anaonekana kujikaza but ana internal demage!!!
 
Nina wasiwasi kama hiyo Jumatatu wataongea hawa na kama wataongea je, watakuwa tayari kusema ukweli kuhusu yaliyowakuta kuanzia walipotekwa mpaka walipoachiwa hiyo saa tisa za usiku. Ni akina nani waliowateka? Waliwapeleka wapi? sababu za kuwateka ni zipi? Na kwanini walichukua TV, camera na vifaa vyao vingine toka studio? Je vifaa vyao vimerudishwa vikiwa salama? Inasemekana mmoja wao message zake za whatsapp zilikuwa zinasomwa je, ni mhusika ndiye aliyekuwa anazisoma au wahuni waliowateka?
Tumepigwa changa la macho, Tanzania hakuna uhuru wa habari.
 
Hivi Tanzania kuna wateja wa hizo vitu kweli , nchi iliyochoka kama hii kuna wa kununua hayo mambo jamani ? Kutoa ni moyo tu mjomba .

Angalia Mzee Mengi anavyotoa hela kwa walemavu .
Mkuu umenichekesha na unanitafutia uchochezi bure hhhhahaha watanzia tuna maneno eti inchi iliyochoka
 
Mimi jana nilipomuona mkewe akizungumza kuhusu Roma nilishikwa na hasira sana. Simjui Roma kihivyo lakini ni Mtanzania mwenzetu ambaye hakutenda kosa lolote yeye na wenzake. Yaliyompata Roma yanaweza kumpata Mtanzania yeyote yule.

Ben Saanane ni zaidi ya miezi sita sasa hajulikani alipo. Sijui kama wameshamuua au bado wanaendelea kumtesa tu. Je kama bado yuko hai wakiamua kumuachia atakuwa ni yule Ben tuliyemfahamu kabla hajatekwa!? Nchi hii inaelekea mahali pabaya sana.

Kinachonisikitisha zaidi ni viongozi wa dini zote kuwa kimya kabisa pamoja na wastaafu kuhusu hii taharuki kubwa sana iliyotanda nchini dhidi ya hii awamu ya tano. Kwanini wanakuwa kimya kiasi hiki hawa? Wanaitekea mema kweli nchi hii? Watanzania wangapi watekwe mpaka waanze kukemea hali hii iliyoleta hofu kubwa sana nchini? Watanzania wangapi watolewe bastola ili waweze kuongea kwa sauti moja kukemea hali hii ya Watanzania kutishwa bila makosa yoyote yale!?

What the regional government is doing to these kids ain't right at all!!! I hope kunasiku wataumbuka oppenly kabisaaaaa!!! This is murder!!!! and the master mind of all these issues is there pretending to help!!! Kweli TU wajinga nimelia kiukweli!!! Kijana wawatu anaonekana kujikaza but ana internal demage!!!
 
Kama leo wanaogopa kuongea kwa sababu ya makubaliano waliyoweka,ikifika jumatatu makubaliano yanaexpaya??
Ina maana hao walioweka makubaliano hawajui kama mtaongea jumatatu???
Ni hatari gani unayoiogopa leo ambayo jumatatu hutaiogopa tena????
wewe huwezi kuelewa kwa sababu uko upande wa watesi
 
R.O.M.A-Rhymes Of Magic Attraction.

Nasubiri wimbo wake kwa hamu this time.Nadhani ataimba mengi mno.Kuanzia kina Bashite,Magari kwenye Kontena,Tumbua-tumbua ya hapa na pale,(Ongezea mengine......)nk.

Lets stay tuned.
 
Vyombo vya dola vya bongo vinatuchukulia poa sana ndo maana watu wanathubutu kwenda nyumbani kwa mtu na kubeba vifaa na kukamata watu bila hata mjumbe kujulishwa-ambapo hata akijulishwa ni kinyume cha sheria kwenda kwa mtu na kupekua na kubeba vitu usiku bila hata search warrant.

Vyombo vyetu vya dola vinatumia mwanya wa watanzania wengi kutokuwa na silaha. Yes! Ukiwa na silaha yako una haki ya kupiga risasi na kuua mvamizi yoyote anayekuja kwako usiku. FBI learnt the hard way about taking matters into their own hands during what is famously known as the Waco Siege.

Kwa kifupi, familia ya mchunguji flani jamii ya kibwetere alikuwa na ranchi yake ambapo waumini wake walikuwa wameleweshwa imani na walikuwa hawaambiliki. Mchungaji huyo pia alikuwa na duka la kuuza silaha. FBI walikwenda kwake bila search warrant, tena mida ya usiku wakiwa wanamtuhumu kwa makosa ya silaha na madawa ya kulevya. Walipoingia kwenye ranchi hiyo sekeseke walilolipata hawatakuja kulisahau maana liliua watu 82 wakiwemo askari na waumini wa jamaa. Na risasi zilipigwa kwa siku 50! Kosa la FBI lilikuwa kwenda kwa jamaa bila search warrant, kama Roma alivyodakwa bila search warrant wala mwenyekiti wa mtaa kujua, Tena unapobeba mali za mtu nyumbani kwake, kimsingi unampekua. Ndugu zangu, sheria inawalinda siku mkikutana na askari wajinga kama hawa, if you are loaded, take them down.

Kwa mengi zaidi kuhusiana na Waco Siege:Raid, fire and rubble: The Waco siege in pictures 20 years on from the cult massacre
 
Kwa nini niliacha kushiriki ibada za kanisani? Kesho tutawaona watekaji wakiwa wameketi viti vya mbele kabisa kanisani kwa 'unyenyekevu' huku watumishi wa Bwana wakiwapa huduma maalum kuliko inayotolewa kwa kondoo wengine waliokaa viti vya nyuma. Pia wanaweza kupewa nafasi ya kusalimia kondoo wenzao na kutumia nafasi hiyo kuongeza hofu na vitisho. Sote tuseme Amen!
 


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Roma akiongea baada ya kutoka hospitali ya Mwananyamala. Amesema yeye na wenzake ni wazima wa afya, kimwili na kiakili na kuwashukuru watanzania wote waliowapigania kipindi cha sintofahamu yao.

Roma amesema kutokana na masuala ya makubaliano yao ya kuachiwa, wameomba kupumzika leo na kesho kisha Jumatatu wataongea kwa kina yote yaliyowapata.


Nitoe tu ushauri katika zama hizi za Kazi za ' Kimafia ' zinazoanza kuota ' mizizi ' hapa Tanzania nadhani afya sana kwa ama Mtu aliyetekwa au Watu waliotekwa pindi wakiachiwa huru tu kuanza kuelezea mipango yao pale pale ya hasa nini watafanya na ni kheri hiyo mipango yao iwe ni ya ' kushtukiza ' tu. Kwa ' Mafia ' na ambao walikuteka halafu wanakusikia unasema kuwa siku fulani utaongea ni ' tiketi ' tosha ya Wao ' kukumaliza ' kabla hiyo siku kufika kwani hawatakubali ' uwaumbue ' au ' uwachafue '. Tujifunze kuwa makini katika mipango yetu hasa Kipindi kibaya cha Kiusalama na cha sintofahamu nyingi hapa nchini na hasa hasa jijini Dar es Salaam.
 
Mhhhhhhhhhhhhh. Hayo makubaliano ya kuachiwa kama yanawabana sasa wasiongee kitu, ninashindwa kujua jumatatu kama wataongea kwa uhuru au wataongea kwa mujibu wa hayo makubaliano ya kuachiwa.

Tanzania my mamaland!. Tunatabasamu nyuso mioyo ikivuja damu. Nadhani amesahau kuishukuru serikali kati ya wale aliowashukuuru kwa kuwapigania.

Ninatamani na Saanane aachiwe kwa makubaliano ya kuachiwa.
Nadhani moja ya makubaliano kuachiwa ni kutokusema ukweli wa kilichotokea! Unakuwa unapewa kitu cha kusema! Unakuwa umetishwa sana! Unaambiwa ukisema utapotezwa jumla!
 
Hili picha hili eti na boss ruge toka asubuhii...manake ruge analijua hili jambo!na kamanda Sirro kaitisha mkutano asubuhi na mikakati kedekede...wanajua wanachofanya HAWA.

Tufanye kazi kwa manufaa ya maisha yetu..sio wa kuwajali HAWA.
 
Namshukuru Mungu kwa kuonekana kwao maaana huku mitaani maneno ya yalikuwa yamesha kuwa mengi kwa serikali. Mungu anaipenda serikali yetu. Hongera JPM kwa kuwa na wapelelezi walio bobea Mungu akubariki aminaa
Wapelelezi waliobobea wameshindwa kumkamata "jambazi" Aliyemtolea Nape bunduki hadharani mbele ya waandishi wa habari na picha yake kuonekana kwenye gazeti la Tz daima ukurasa wa mbele! Kweli wamebobea!
 
Roma anaonekana kuteswa sana!amevimba pia,anachechemea japo kasema yeye ni mzima
Inaniumiza sana!
Millard ayo amepost insta na cloudfm pia wamepost clip ya video alipokuwa anashuka kwenye gari,,kweli siyo mzima japo anajaribu kutuaminisha hivyo!
Huenda hataki kuumiza hisia za mashabiki zake,ama amekatazwa kusema kuwa ni mgonjwa!
 
Back
Top Bottom