Huo wimbo ni wa zamani sana enzi za Beni Bati. Hizo zilikuwepo sana miaka ya 1960s na 1970s, nadhani wengi wa wana JF hamkuzikuta hizo. Zilikuwa ndiyo kama miduara ya sasa, zikiongozwa na beni (band) kusindikiza arusi n.k. Labda kama enzi hizi wanavyofanya matarumbeta. Arusi msururu wa magari ulikuwa ukisindikizwa na beni, au mdundiko, hasa Dar es Salaam sijui miji mingine. Nyimbo ziko nyingi lakini huo ulikuwa mmoja wapo uliokuwa maarufu sana enzi zile. Zingine kama 'Mwanionea mpenzi mwenyewe hayupo, mola akipenda mpenzi atamrudisha' pia zilikuwa maarufu sana kwa beni bati. Kahistoria karefu kidogo wana JF, Jay Dee na wana njenje na wengine wanazirudia tu hizo nyimbo.