Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Mtangazaji wa Kituo cha Runinga cha KBN nchini Zambia amefunguka kuwa yeye na wenzake hawajalipwa mishahara yao.
Kalimina Kabinda alikatisha taarifa ya habari na kuwaumbua waajiri wake mubashara, na kisha kuichapisha video hiyo katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
Pamoja na video hiyo, Kabinda aliandika, “Ndiyo, nilifanya hivyo kwenye matangazo mbashara ya TV kwa sababu waandishi wengi wa habari wanaogopa kuongea, haimaanishi waandishi wa habari hawapaswi kuongea.”
Baada ya video hiyo kuzua gumzo, Mkuu wa Kituo hicho cha Runinga, Kennedy Mambwe alimlaumu Kabinda akisema alikuwa amelewa wakati alipokuwa akisoma taarifa ya habari, lakini hakuzungumzia madai yake.
“KBN ina mfumo mzuri wa kuwasilisha malalamiko ya wafanyakazi wake, hivyo tabia ya Kabinda ni kinyume na maadili tunayosimamia kama Kituo,” taarifa ya Mkuu wa Kituo hicho ilieleza, ikitaja kuchukua hatua za kuwanidhamisha wote wanaohusika.