Video: Mvua kubwa ilivyosababisha athari mitaa ya Mwanza, leo Desemba 10, 2023

Mikoa yote mikubwa kuanzia DAR,mwanza na Arusha miundombinu yake inafanana Tu kwakifupi Tanzania inahitaji maombi tu
 
Inashangaza ziwa lipo karibu kuweza kuelekeza mifereji huko ili kukabiliana na mvua kama hizi.

Inashangaza ziwa lipo karibu kuweza kuelekeza mifereji huko ili kukabiliana na mvua kama hizi.
Hayo maji yanaelekea hukohuko kwani ziwe lipo lowest kwenye lowest level ya kwa hapo mjini. Tatizo la hayo mafuriko kuna mdau kaelezea hapo juu
 
'Hakuna mafuriko, watu wanafuata makazi [na mapito ya maji]'
Chalamila.

Tusipotii sheria za mipango miji, maji yatatutesa miaka yote.
Kwahiyo mji wote wa Mwanza uvunjwe yaachwe maji tu?
Vipi kuhusu Hanang watu pia wamefuata njia ya maji? Ukitembea Ulaya mito inapita katikati ya mji na hakuna haya mafuriko
 
Kwahiyo mji wote wa Mwanza uvunjwe yaachwe maji tu?
Vipi kuhusu Hanang watu pia wamefuata njia ya maji? Ukitembea Ulaya mito inapita katikati ya mji na hakuna haya mafuriko
Kwani mji wote wa mwanza ni sehemu ya wetlands?

Umesema vyema ulaya. Unaelewa maana ya kuheshimu mipango miji?
 
Hiyo mvua ni kubwa sana hata mngekuwa na miundombinu mizuri bado hali ingekuwa tete
 
Mitaa ya Coconut Hotel ndio huwa iko jirani kabisa na mto kenge (umepita nyuma yake), kuna mzee wangu mmoja ana workshop ya welding mitaa hiyo, jana hapakukalika.
 
Narudia kusema huo mto mirongo alimaarufu mto kenge ungekuwa msafi na umejengelewa kwa kuta imara harafu madaraja yawe mapana kwa mvua ya jana isingeleta kizaa zaa hicho
Ila miundombinu ni ya hovyo sana na mto umebanwa na uchafu
So maji yanajitafutia tu njia ya kupita
Hiyo mvua ni kubwa sana hata mngekuwa na miundombinu mizuri bado hali ingekuwa tete
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…