Video na Picha: Ushahidi kuhusu yaliyotokea kwa Jaji Warioba wakati na baada ya vurugu, Ubungo Plaza

Video na Picha: Ushahidi kuhusu yaliyotokea kwa Jaji Warioba wakati na baada ya vurugu, Ubungo Plaza

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,171
Reaction score
23,996
Jamiiforums is where we dare to talk openly!



Kwa mwananchi yeyote ambaye hajafungwa kimawazo na kifikra, angalia vizuri hii video kwenye dakika ya 1:18 ili yale uliyoambiwa uchanganye naya kwako kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwa Paulo Makonda!.

Pix-1.JPG


Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba Inayopendekezwa, Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam.
DSC_2016.JPG

Jaji Joseph Warioba akitoa mada katika kongamano kabla ya vurugu kutokea.
Pix-2.JPG

Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakionyesha mabango yao.
Pix-4.JPG

Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa na mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba Inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.


Pix-3.JPG

Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya kuanza vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba Inayopendekezwa.


Pix-5.JPG

Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole akiongea na mmoja wa vijana aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba Inayopendekeza.

Pix-6.JPG

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba Inayopendekezwa.


DSC_2069.JPG


DSC_2072.JPG

Baadhi ya vijana wakionyesha mabango yenye ujumbe mbali mbali
DSC_2135.JPG

Paulo Makonda akimsaidia mlemavu wa macho, Amon Mpanju baada ya vurugu kuanza kutokea ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza.
DSC_2163.JPG


DSC_2181.JPG

Baadhi ya viti vilivyotumika kama silaha na kinga kwenye vulugu

DSC_2263.JPG

Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu.
DSC_2268.JPG

Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa
Pix-4.JPG
 
Taifa letu litaangamizwa na unafiki na uwongo wa baadhi ya watu wanaofaidika au wanaodhani watafaidika na matokeo ya unafiki na uwongo wao.

Ukweli hutafutwa.

Ukweli huweka huru kila binadamu anayeutafuta na kuupata.

Hotel ina CCTV, ukumbi pia una CCTV.

Ukweli hutumia ngazi wakati uwongo hupanda lift.

Kuna baadhi ya wananchi wanawaza katika mlengo wa hisia, wanaongozwa kwa hisia na wanaishi kwa hisia.

Ukweli umeanza kutufikia kwa sasa.
 
Hahahaha......ACT mzigoni......maisha haya......
 
Naona mmeanza kuupaka upepo rangi sasa! Makonda ndiye alieratubu vurugu hizo! Yeye na mdogo wake Nchemba anaeonekana hapo ndiyo chanzo cha Vurugu na kumpiga mzee wetu! Watoto hawana adabu hata kidogo! Laana ya wazee wetu itawadhuru hadi kwenye makaburi yenu ... Grrrrrrr
 
Taifa letu litaangamizwa na unafiki na uwongo wa baadhi ya watu wanaofaidika au wanaodhani watafaidika na matokeo ya unafiki na uwongo wao.
hao vijana walioleta fujo ni wasaliti na maadui wa taifa. kama serikali haitawachukulia hatua, si wanaonekana kwa sura, wanajulikana tunao huku mtaani, kwanini tusiwafuate hukuhuku mtaani tuwale kabang ili iwe fundisho kwa vijana wengine wanaotumiwa? nchi hii ya kipumbavu sana.
 
Ujinga mtupu!

Sasa ni nini hiki? Mimi nilidhani hiyo clip itamwonesha mtu anayerusha jiwe. Kumbe kilichofanyika hapa ni TBC kuondoa picha ya Paulo Makonda wakati akimrushia jiwe jaji Warioba. Pathetic CCM.

Ningeshangaa sana kama TBC ingeweza kuonesha kitu kilichotokea wakati sasa chombo hiki kimebakia kuwa ni chombo cha propaganda cha CCM. Nchi ikirudi kwa wananchi, chombo hiki kinachokula kodi yenye bila faida yoyote itabidi kuvunjwa na kuanzishwa upya kikiwa na malengo mapya na maongozi mapya. Na nadhani uongozi wa juu uliokwishachafuliwa na CCM, wote itabidi kusafishwa.
 
Kuna kitu kinapikwa, tunafichwa na hakiko wazi. Team ya uchafuzi ya chadema iko kazini. Kama kweli MAKONDA kafanya haya, basi hukumu ya mungu dhidi yake haiepukiki. Ila kama ndio ileile style ya CHADEMA ya kuwachafua vijana wana mapinduzi,,, basi MAKONDA atatoka katika hili kama shujaa.

Nawakumbusha tuuu.

YU WAPI YULE ADUI MKUU WA CHADEMA MWINGULU NCHEMBA)
YU WAPI YULE ADUI WA KUDUMU WA CHAMA(ZZK)
YU WAPI ADUI MWINGINE WA CHADEMA ((JAKAYA MRISHO KIKWETE)
nionavyo mimi, yule aliye adui mbele ya CHADEMA ni TUNU ya taifa letu. Tusubiri, hata makonda itathibitisha hili.
 
Makonda amejibu uzushi unaosambazwa mitandao tangu jana kuwa kampiga mzee Wariyoba

"Mimi nilienda kama Mtanzania mwingine yeyote wa kawaida ila vijana waliponyoosha mabango walitokea watu waliyotaka kumdhuru mlemavu wa macho nilitokeza kumsaidia baada ya hapo nilimsaidia pia mzee wariyoba zipo picha mtaziona"


Ukumbi wa ubungo plaza ni ukumbi wa kisasa sana una camera pande zote hilitukio liangaliwe vizuri mtaona kama nimefanya hilo tukio hilo

Chanzo ni radio free Afrika.
 
Back
Top Bottom