Video: Ndege ya American Airlines yasimama ghafla baada ya tairi la ndege kuwaka moto

Video: Ndege ya American Airlines yasimama ghafla baada ya tairi la ndege kuwaka moto

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Abiria wa ndege ya American Airlines walilazimika kuteremka kwa kutumia milango ya dharura katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Denver baada ya tairi la ndege kuungua wakati wa jaribio la kupaa.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 MAX 8 yenye abiria 173 ilitarajiwa kuelekea Miami. Abiria mmoja alipelekwa hospitali kwa majeraha madogo, huku wengine watano wakikaguliwa na madaktari eneo la tukio.

Video iliyorekodiwa na abiria ilionyesha ndege ikianza kasi kabla ya kusikika mlipuko, mtikisiko mkali na tairi likionekana likiendeshwa pembeni mwa barabara ya kurukia ndege. Harufu ya moto ilisababisha abiria kupiga kelele na milango ya dharura kufunguliwa.

===========================

Passengers evacuated an American Airlines jet at Denver International Airport on emergency slides after the landing gear caught fire during an aborted takeoff, sending black smoke billowing into the air.

One of the 173 passengers was hospitalized with minor injuries while exiting the Boeing 737 MAX 8 that had been due to fly to Miami International Airport on Saturday, according to officials.

A video shared with NBC News by a passenger, who wished to remain anonymous, showed the aircraft gathering speed on the runway

before a loud bang was heard followed by strong vibrations and the plane stopping. Meanwhile a round piece of debris was seen rolling from underneath the plane and off the side of the runway.


Source: NBC News
 
Back
Top Bottom