Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Ahsante kwa kunirekebisha.
kiranga,
Unafikiri ni kwanini vyombo vya ulinzi vinatumiwa kufanya kazi chafu tofauti na miiko yake ya kazi?
Sheria zinawalinda vipi askari wa chini kutambua kwamba hii ni “abuse of power” na si “chain of command”?
Zipo sheria zinazowapa uhuru wa kupinga kwamba hii ni abuse of power hivyo siwezi kutii?
Rais wa zamani wa Burkina Faso, Captain Thomas Sankara aliwahi kusema kwamba, askari ambaye hana elimu ya kizalendo ya siasa anaweza kuwa mhalifu tu.
Nukuu yake ni hii "Without patriotic political education, a soldier is only a potential criminal.”
Mwanajeshi wanatakiwa kupewa elimu ya siasa, ya uraia, ya uzalendo, ya falsafa, ya mantiki, ajue maadili, ajue amri halali na isiyo halali.
Kuna sheria kama whistleblowers act zinamlinda askari kufanya kitu cha njama zisizo halali, lakini hata akilindwa na sheria, in practice ni vigumu sana ku survive hususan nchi zetu za Africa.
Ila sasa, kwa mfano kama Kenya, mwanajeshi akikataa kuua raia halafu raia wakabadiki utawala, mwanajeshi yuko safe. Ila mwanajeshi akikataa kuua raia halafu utawala uendelee ule ule, mwanajeshi anaweza kupata matatizo.
Egypt wanajeshi walikataa kutii amri za rais Hosni Mubarak kuua raia, lakini Mubarak akaondoleea wanajeshi wakawa salama.