Mimi binafsi naona watu mnaomsema Mzee Wasira ni kwasababu mnamuogopa!
Mzee huyu ukimlinganisha na rais wa Marekani Donarld Trump mzee Wasira bado ana nguvu sana japo kamzifi mzee Trump mwaka mmoja.
Watu ambao wanaogopa nguvu ya kujenga hoja zinazotokana na uzoefu alionao Mzee Wasira kutokana na kukaa ndani ya chama na serikali kwa muda mrefu sana ndio kila siku kumsemasema kama vile hamna mazungumzo mengine.
Mzee Wasira bado Yuko fiti sana na CCM hawakukurupuka wala hawakukosea kumpa mzee Wasira nafasi hiyo!.
Kumbukeni palipita muda mrefu sana tangu mzee Kinana ajiuzulu kwahiyo walipata muda wa kutuliza akili na kuwakagua makada wa CCM mmoja baada ya mwingine hadi mwisho ndio wakaona ni mzee Wasira ndiye mtu sahihi anayefaa kwa nafasi hiyo kutokana na hali iliyopo ya joto la kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu!.
Kwahiyo tulieni na bado hamjasema, yaani lazima mseme!