Video: Nimekuwa Mtanzania wa kwanza kuvuka Ubungo flyover tokea Mlimani City kuelekea Riverside

Nadhani hapa sasa Tanzania kama nchi tunaweza kuanza kuvuna matunda ya hili daraja, maana loss tuliyokuwa tunaingiza kwenye foleni za Ubungo kama taifa, ilikuwa kubwa mno!! Ona video.

Kwaio tukuchinjie jogoo la njiwa ama...? [emoji848]
 
Hawa watu kwanini wanakimbia nchi yao? Wana mradi wa reli ya SGR mkubwa kuliko yote barani Afrika. Wana mradi mkubwa wa umeme. Picha ya chini ni moja ya flyover zilizopo mjini Adis Ababa. Wana shirika kubwa la ndege kuliko mashirika mengi barani Afrika. Haka ka 'airbus' kamoja tunakojivunia nako, wao wanazo 45, achilia mbali utitiri wa Boeing, Bombadier na ATR.

Wana mradi mkubwa wa umeme uitwao GRHEP ambao unazalisha karibu megawati 9,000. Mradi huo ni mkubwa karibu mara 5 ya mradi wetu tunaojisifia nao wa "Stiglers gorge" ambao utazalisha megawati 2,000 ukikamilika. Ethiopia wa kwao ni 9,000MW. Wana viwanja vya ndege vya kisasa.

Lakini kila siku watu wanatoroka nchini kwao kukimbilia ughaibuni. Wanasafirishwa kwa magari ya mizigo. Wengine wanazamishwa kwenye magunia ya pumba vichwa tu vinatokeza nje. Wengine wanasafirishwa pamoja na mifugo.

Lakini kwanini mtu aache barabara za lami, flyover, madaraja, viwanja vizuri vya ndege, na akimbilie nje ya nchi na kukubali kusafirishwa pamoja na mifugo? Jibu ni kwamba MAENDELEO YA VITU hayawezi kuwa muhimu kuliko MAENDELEO YA WATU.

Ukijenga Flyover wakati mama anakufa kwa kukosa dawa hospitalini means umethamini vitu kuliko watu. Ukijenga Terminal viwanja vya ndege hadi kijijini kwako wakati vijana hawana ajira na umezuia serikali kuajiri means unathamini vitu kuliko watu.

Ukijenga bwawa la umeme wakati hujapandisha mishahara ya watumishi kwa miaka mitano means unathamini vitu kuliko watu. Ukijenga reli wakati wakulima wa korosho na mbaazi wanahangaika kupata soko means unathanini vitu kuliko watu.

Sijasema tusijenge reli, wala flyover. Tujenge lakini tuwe na vipaumbele. Kuna faida gani kujenga reli kama kuna mama kule Namtumbo anakufa kwa kukosa dawa ya bei rahisi tu? Kuna faida gani kununua ndege kama kuna watu wanakunywa maji machafu ambayo wanayatafuta kilomita 20 kutoka walipo?

Ni baba mpumbavu pekee anayeweza kusifiwa kwa kumnunulia mkewe Iphone X lakini aliacha mwanae akafa kwa kukosa laki moja ya matibabu.
*Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8[1](a) inasema "Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa (wananchi) WATU sio ustawi wa VITU. Asomaye na afahamu.!*
 
Ila maendelea ya vitu ndio yataleta maendeleo ya watu, hivi viwili vinategemeana, vitu ndio vitaendeleza watu
 
Mkuu pia tunazungumzia shule bora sio hizi ambazo hazina walimu wa kutosha hazina madawati hazina maabara na vifaa vya kufundishia watoto wanafaulu kwenda kidato cha kwanza hawajui kusoma na kuandika, sio hizi hospitali ambazo hazina dawa wala vifaa tiba, hakuna aliyesema vitu visijengwe lkn maendeleo ya watu ni muhimu zaidi

unajenga barabara lkn hakuna ajira kwa miaka 5 hizo sio akili
unajenga barabara unashindwa kupandisha moshahara watumishi wa umma na unakataa kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa sheria
unajenga mabarabara huku unadhurumu wakulima kwa kuwakopa na kutokuwalipa kwa wakati
unajenga barabara huku unatoa mikopo ya elimu ya juu kwa upendeleo....

HIZO HAPO JUU NI AKILI MBOVU SANA
 
Huu uzinduzi kiboko. Alitanguliwa na wakenya na uganda. Pembeni wahindi walikuwa na bajaji
 
Watanzania Wengi Tumemchoka magufuli.

Mbingu yote Imemkataa.
Hakataliwi kwa mwangwi wa mitandao, kamkatae Trh 28'uko!

Hivi kwa maneno hayo, akishinda kihalali mtasema kakwiba matokeo?

Tusijiachie sana kujiaminisha fikra zetu, maana lolote laweza kutokea halafu ikawa aibu ya kubadili hadi 'profile'.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hapa sasa Tanzania kama nchi tunaweza kuanza kuvuna matunda ya hili daraja, maana loss tuliyokuwa tunaingiza kwenye foleni za Ubungo kama taifa, ilikuwa kubwa mno!! Ona video.

Akili ndogo ni sumu ya mwili . Ushamba mzigo ndugu yangu pole sana kuwa na vyotee
 
Ukiwa huko juu nikajua upo Alabama ila uliposhuka tu picha likabadilika nikatambua upo kwenye nchi ya rais mustafu wa dar, his malevolent bashite
 
Naona na simu iligeuzwa ili kuchukua taswira ya aliyelijenga daraja kwa hela zake!
 
Back
Top Bottom