Video: Performance ya Marioo kwenye tuzo za Trace ina shida gani? Kwanini mnasema kaaibisha taifa?

Video: Performance ya Marioo kwenye tuzo za Trace ina shida gani? Kwanini mnasema kaaibisha taifa?

Sio shabiki wa Kiba ila kususia haya maonesho alinifurahisha..licha ya ukweli kwamba performance yake ingekuwa mbaya kuliko zote😂😂
Alichungulia akaona pamoto.
 
Wasanii wa Tanzania wana uwezo mzuri wa kutunga muziki mzuri sana. Shida inakuja kuimba live hawafanyi mazoezi ya kuimba.

Kikawaida alitakiwa awe na team ya performance waanamua ni nyimbo zipi zinafaa kuimba kwenye jukwaa kubwa. pia wanatakiwa kuimba mwanzo mwisho. Na wanatakiwa kuwa na mwalimu wa kuwafundisha kuimba jukwaani kama kwaya za shule au za kanisani. Wenzetu wanafanya hivyo sio kwamba hawajui kuimba live wanajua ila wanataka kuwapa mashabiki performance nzuri sana.

Hio ya ye yoo inua mikono juu sema waa weee ni ya sehemu ambazo sio rasmi au wakitoka out na marafiki zao.

Sasa kama arena itajengwa kwa ajili ya matamadha makubwa sisi watanzania situtamezwa na Nigeria na Kenya?.
 
Wasanii wa Studio, nje ya hapo hawana kitu cha kuonyesha.
 
Ukitizama perfomance za kina Chris Brown kama ile amefanya SA, utagundua bongo bado tunacheza..
 
Wapambe wake na jamaa zake wa karibu.

Watakuwa wanamjaza kwamba ametisha, kwenye stage, ameua, amekamua kinyama.

Ni mwendo wa kupapasa ego, wapate chambi chambi.
 
Back
Top Bottom