Wasanii wa Tanzania wana uwezo mzuri wa kutunga muziki mzuri sana. Shida inakuja kuimba live hawafanyi mazoezi ya kuimba.
Kikawaida alitakiwa awe na team ya performance waanamua ni nyimbo zipi zinafaa kuimba kwenye jukwaa kubwa. pia wanatakiwa kuimba mwanzo mwisho. Na wanatakiwa kuwa na mwalimu wa kuwafundisha kuimba jukwaani kama kwaya za shule au za kanisani. Wenzetu wanafanya hivyo sio kwamba hawajui kuimba live wanajua ila wanataka kuwapa mashabiki performance nzuri sana.
Hio ya ye yoo inua mikono juu sema waa weee ni ya sehemu ambazo sio rasmi au wakitoka out na marafiki zao.
Sasa kama arena itajengwa kwa ajili ya matamadha makubwa sisi watanzania situtamezwa na Nigeria na Kenya?.