DOKEZO Video: Trafiki wa Bahi wanamtia doa Rais Samia, wachunguzwe

DOKEZO Video: Trafiki wa Bahi wanamtia doa Rais Samia, wachunguzwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Polisi akili zao ndogo sana,sasa funguo anachukua ya kazi gani?
 
Hawa maaskari kutoka Bahi wanakera sana, unalazimishaje kuingia kwenye gari ya mtu na kutaka kuchomoa funguo? Gari yenyewe hata kukukimbia haiwezi, gari ina mali za mamilioni ya wafanyabiashara.

Rais kupitia kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, sisi madereva tunakuomba uunde timu ya uchunguzi kufuatilia nyendo za Askari Trafiki wanaohudumu katika eneo hili la bahi. Wamejaa ubambikizi, ubabe, Rushwa na manyanyaso kwa madereva.

Sasa askari na mamlaka yote uliyonayo unashindana na kujibizana na dereva kama vile na wewe ni mpiga debe, iko wapi heshima na nidhamu ya jeshi la polisi?

Mwisho ukiona mpaka inafikia hivi dereva kuamua kulete vurugu hivi basi tutafakari kuwa kuna jambo halipo sawa mahala husika, hata hivyo malalamiko ni mengi sana kuhusu eneo hilo.

Swali la kujiuliza hapo ni kwanini Bahi tu na siyo Manyoni, Tinde ama Gairo? Kwani huko kote hakuna maokoto, si yapo na amani imetawala? Kinacholalamikiwa ni kuwa hapa kuna maokoto ya kulazimishwa, siyo yale ya fairplay.

Kwako Madam President,
Nakala kwa Mh. Masauni,
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Kamanda wa Trafiki nchini.

Sasa hii Mali iliyobebwa ikipata shida huyu traffic atamudu gharama?

Afukuzwe kazi right away
 
Back
Top Bottom