The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Kitabu chake "REMAINING IN THE SHADOWS: PARLIAMENTS AND ACCOUNTABILITY IN EAST AFRICA" kinachambua historia (history), mapungufu (weaknesses) na mazuri (strengths) ya mabunge ya nchi zote mama za Afrika Mashariki i.e Kenya, Tanzania na Uganda...
Ameanza kukiandika kitabu hiki mwaka 2020 na kukimaliza mwaka huu 2021 na kisha kukizindua wiki iliyopita huko Nairobi, Kenya...
Katika video hizi mbili, moja hapo juu na ya pili hapo chini anaeleza sababu za kuandika kitabu hiki, maudhui kuu ya kitabu (the central theme) na kwanini amezindulia kitabu hiki Nairobi - Kenya na siyo Tanzania.
Huyu ndiye Tundu Lissu, mwanasiasa na mwanaharakati wa haki za binadamu asiyeweza kuzuiliwa wala kunyamazishwa na kitu chochote ili kusema au kuandika chochote anachoamini ni sahihi.