Video: Uchawi haupandi ndege, juju la Simba halikuzaa matunda Johanesburg

Aibu ya Taifa hii! Halafu bado walifungwa. Kipinde kile na FC Platinum, waliingia na Paka!

Simba bhana! Yaani wameturudisha kwenye Vita ya Majimaji ya mwaka 1905-1907! Wanaamini katika karatasi yenye maandishi ya 'Kiarab' bila shaka, ili kuvuka hatua ya nusu fainali!
 
Nachukia kweli huu upuuzi kwenye michezo. Turoge mengine lakini sio michezo
Mie nachoonaga kuwa kweli wazungu wanasema ukweli kuwa sie ni manyani ni pale ambapo uchawi wetu tunaelekezeana wenyewe kwa wenyewe waafrica baadala ya kumroga mzungu🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kwa kweli aibu nimeona mimi. Kwenye zama hizi za teknolojia hivi unafanyaje mambo ya hovyo kiasi hiki mbele ya kamera zinazorusha matangazo dunia nzima. Simba wajiandae tu kwa rungu la CAF. Mambo ya hovyo hivi kwenye dunia ya leo hata kwenye ligi yetu hayafai.

Kuna haja gani sasa ya kuhangaika kusajili wachezaji toka Malawi, Kenya, Uganda, Zambia, Ghana, na kwingineko ili hali unaweza tu kusajili waganga wa kienyeji wa kutosha. Kuna haja gani ya kuajiri benchi la ufundi lililojaa wazungu na mpaka una mtu wa kutathimini mchezo wa mpinzani wako halafu unaenda kuloga kifala hivyo.

Ombi langu ni kuwa yoyote yule aliyeshiriki huo upuuzi awe Mo, Babra, Kaduguda, n.k ajiuzulu mara moja na ajiondoe Simba. Haiwezekani timu iliyojijengea heshima Afrika kwa takribani miaka minne sasa halafu inajishushia heshima kijinga hivyo. Hata kama kuna amsha amsha basi zingefanywa kwa siri sio hadharani kiasi kile kiasi zinataia aibu taifa na watanzania kwa ujumla.
 
Hii nahisi ni siku wanafanya mazoezi na sio jana.
 
Kwa kweli aibu nimeona mimi. Kwenye zama hizi za teknolojia hivi unafanyaje mambo ya hovyo kiasi hiki mbele ya kamera zinazorusha matangazo dunia nzima. Simba wajiandae tu kwa rungu la CAF...
Kwa kweli caf wameshusha hadhi ya haya mashindano. Unaruhusu vipi kitu kama hicho kutokea katikati ya uwanja?
Dawa pekee ya vitu kama hivi ni kuifungia timu kutokushiriki mashindano na sio fine wanazotoa.
 
Nadhani ni mind games kama yule kipa alivyokuwa anamchimba mkwara kapombe "Is you again??"
 
Kwa kweli caf wameshusha hadhi ya haya mashindano. Unaruhusu vipi kitu kama hicho kutokea katikati ya uwanja?
Dawa pekee ya vitu kama hivi ni kuifungia timu kutokushiriki mashindano na sio fine wanazotoa.
Kuna ofisa mmojawapo pale alikuwa anachukua ushahidi. Adhabu zao zinakuja baada ya muda. Kama utakumbuka Berkane waliadhibiwa baada ya muda fulani kutokana na vurugu walizofanya hapa Dar.
 
yaani uje na fake id yako uandike utumbo halafu ushinikize watu wajiuzulu nyani shida sana
 
Simba bila kutumia uchawi,ni 0 kabisa...
 
Uchawi haufanyiki hadharani hivyo... walikua wanajifukiza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…