The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, leo jumapili ya Novemba 30, 2025, wameendelea na ibada za kila jumapili, ikiwa ni jumapili ya kwanza tangu Kanisa hilo kuruhusiwa kuendelea na shughuli zake baada ya kuzuiwa kwa muda.
Novemba 24, 2025, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, alitoa tangazo rasmi la kuruhusu waumini wa kanisa hilo kuendelea na shughuli zao, ikiwa ni baada ya kufungiwa Juni 2, 2025.
Na Novemba 25, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Albert Msando, alikutana na uongozi wa kanisa hilo na kuwaruhusu rasmi kuendelee na shughuli zao za kidini.