jamani jamani, mimi sipendi kuwacheka hao wasanii kwani ninaamini kabisa hicho kingereza walichoongea ndio wanachokifahamu. pia muelewe kuna presha ya kujua unahojiwa mbele ya kamera tena katika lugha ambayo si yako ulikokulia zaidi ya kujifunzia ukubwani nayo inachangia kidogo kusahau hata maneno wanayoyafahamu.
pili baadhi yao kiwango cha elimu walichonacho kinachangia, tutambue fika si Watanzania wote waliopita katika shule za English Medium, na baadhi tuliosoma shule ya chini ya mwembe na madarasa ya nyasi, hakuna vitabu, kuna upungufu wa walimu, matatizo ya ada na matatizo mengine ya kifamilia aliyokumbana nayo huyo msanii mpaka kufikia hatua hiyo ya kujikomboa kwa kutumia kipaji alichopewa na Mungu kufikia hapo leo. la msingi ni kuwahimiza hao vijana (wasanii) kujiendeleza kielimu hata kwa kwenda katika madarasa ya jioni ya kujifunza lugha za kigeni mfano kiingereza ama kifaransa ili usanii waweze kuuza kazi zao kwa kiwango cha kimataifa, ninaamini tukiwapa muda wakajiendeleza baada ya miaka kama miwili ninahakika tukija kukutana nao katika hayo mahojiano ya kimombo nao watakuwa wanaelewa na kuongea kiufasaha tena huenda kuliko hao wanavyoongea leo hii.
aidha, tutambue si wasanii pekee ambao lugha za kigeni zinawapa shida jamani ni kila kada kuna tatizo hilo kwahiyo leo wakianza kunyolewa hao wengine twendeni shule sio kuwashikia mabango kama wametenda kosa la jinai, ongeeni nao kwa kiswahi ama lugha zao za asili mtawaona kama watababaika.
mwisho mimi ninawapongeza sana wasanii wote wanaojituma na hata kufikia mafanikio ya kuitangaza nchi yetu ya Tanzania katika ngazi ya kimataifa ial wajue umaarufu una gharama zake na ili kweli udumu katika huo umaarufu na usiwe mbabaishaji basi warudi shule kama wafanyavyo baadhi ya wasanii wenzao jamani dunia ya leo si ya kutumia vipaji na ujanjaujanja tu tutaporomoka ni shule na hayo mengine ni ya ziada kaka na dada zangu.