Video: Vuta Nikuvute ya Halima Mdee, Spika Tulia na Patrobas Katambi kuhusu Mkataba wa DP World na Serikali

Video: Vuta Nikuvute ya Halima Mdee, Spika Tulia na Patrobas Katambi kuhusu Mkataba wa DP World na Serikali

Upinzani wa kukulupuka usio na facts..
Leo umetambua akina Halima mdee ni wapinzani. Huyo Tulia kabakia kuhoji vimaswali uchwara kisa Halima anaongea. Kwanza anaonesha ana upande na hataki mtu abishe. Hongera halima kwa leo Rudi nyumbani.
 
Sasa kati ya Tulia na Halima nani msomi wa kukariri?

Huyo halima anaongea mambo ambayo anaulizwa yapo wapi kwenye mkataba anashindwa hata kuyaonesha ndo unamfananisha na Tulia?
Alichokifanya Spika ni interruption technic ambayo hata yeye akishtukizwa angepotea uhalisia upo hivi mkataba haupo specific upo open ended unaweza chukua kila kitu. Huu ni mkataba wa kihuni kuliko yote iliyokwisha fanywa na bunge hili. Mkataba unawalinda sana wageni na kutoa ardhi ya nchi kwa wageni, na kuingilia utendaji wa bandari na usalama wa Taifa
 
Je kazi ya spika ni kubishana na mtoa mada? Kama alivyofanya? Mdee alikuwa anaongea na spika au wananchi wa Tanzania? Je hizo taarifa za kipuuzi ni sawa kwa nini spika asimlinde mzungumzaji? Je watanzania ni wajinga kiasi hiki? Poor tz
 
Najua bunge litaupitisha ulivyo ila Serikali kwa utashi wao waupitie upya na kuurejebisha kwa maskahi mapana ya nchi. Historically hii kampuni imeishia kuingia matatizoni na nchi nyingi sana duniani kuna cha kujifunza hapa. Hata usingepitishwa bungeni au kuvuja kwa wananchi bado hili litahojiwa na viongozi wajao na kutuona watz wa sasa tulipotoka na kutokuwa na uzalendo.
 
Huyu spika anatoa muda kwa mbunge kuchangia halafu anaanza kufanya interruption...........hivi kwa nini nguvu kubwa sana inatumika kulazimisha hili jambo.

Jana yule bush doctor alijikita kuzungumzia ufanisi duni wa bandari kama kigezo cha kuuza kwa mwarabu na kwamba mapato yatokanayo na bandari ni pesa kidogo sana. Lakini huyu bush doctor ameshindwa kuelewa kuwa tatizo la nchi hii siyo mapato bali ni ufisadi uliopindukia na matumizi holela ya pesa za umma.

Hii maana yake ni kwamba unataka ku compromise usalama wa nchi kiulinzi na kiuchumi ukilenga kupata mapato makubwa yatokanayo na bandari ambayo kimsingi hayana msaada wowote kutokana na ubadhirifu na matumizi holela ya pesa za umma. Hayati Magufuli aliwahi kukiri kwamba nchi hii ina pesa nyingi sana hadi kuipa hadhi ya kuweza kuwa donor country.

Kwa hiyo point ya msingi iliyopo hapa ni kwamba bandari inamilikishwa kwa wageni jambo ambalo ni hatari kwenye usalama wa nchi na ulinzi wa rasilimali zetu yakiwemo madini na wanyamapori. Swala la ufanisi linaweza kufanyiwa kazi na TPA kwa ubia na kampuni za kitanzania au kampuni za nje lakini si kwa mkataba unaotoa umiliki wa bandari kwa wageni.​
 
Back
Top Bottom