VIdeo: Wabunge wa Marekani waandamana hadi mbele ya jengo la USAID wakitaka misaada irudishwe haraka, wataka Elon adhibitiwe!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Huko nchini Marekani, viongozi na baadhi ya wabunge wameandamana nje ya jengo la USAID wakitaka shirika hilo lirudishwe na misaada irudi haraka sana.

Jamii Raskin ambaye ni mbunge kutoka jimbo la Maryland aliongozana na wabunge wengine wakitaka shirika hilo LIRUDISHWE na Elon Musk asijihusishe na shughuli zozote za kiserikali.

"Elon Musk hukuitengeneza USAID, Marekani kupitia bunge ilifanya hivyo kwa ajili ya Wamarekani. Hana nguvu ya kuiharibu (USAID) na nani ataenda kumdhibiti (Elon)? Ni sisi hapa. Hatuna mhimili wa nne wa serikali unaoitwa Elon Musk"

===================

Elon Musk sio mbunge wala hajachaguliwa na wananchi wa Marekani kwanini Trump anampa mamlaka makubwa sana na hajachaguliwa wala kupitishwa na bunge?

Your browser is not able to display this video.
 
Huyo muhamiaji kutoka South Africa Elon Musk anawapelekesha balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…