MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Ni dhahiri kwetu hapa Kenya tuna changamoto zetu, hamna taifa lisilokuwa na kasoro, pia tuna migawanyiko yetu na mara nyingi huwa tunakubali kutokubaliana, ila kwa wenzetu Tanzania ukifuatilia siasa zao, unajiuliza mbona waharibu hela nyingi hivyo kufanya kampeni za maigizo zisizokua na umuhimu wowote kidemokrasia.
Watu wanaambiwa bila kufichwa wakichagua wabunge wa upinzani basi wasahau maendeleo, wasiagize maji wala nini, wengine wanapigwa mikwara kwa kilugha, ishara za ukabila uliopitiliza.
Siasa za Tz hunikumbusha ilivyokua wakati tukiwa watoto mtaani, mwenye mpira ndiye alikua anaamua magoli yawe vipi, akina nani wawe kwenye timu yake, na mchezo utachezwa kwa muda gani, akichoka anautia kwapani na kwenda kwao nyumbani.
Jameni mashujaa tuliopambana mpaka tukapata katiba mpya tutembee kifua mbele siku zote, tutawaachia watoto wetu urithi wa maana sana, inawezekana vizazi vya kesho visije kujua jitihada na mateso tuliopitia hadi kuipata hii katiba, lakini mwisho wa siku kama mzazi, unaachia wanao urithi mzuri bila kujali watautumia vipi.
Video hii hapa... https://www.jamiiforums.com/data/attachment-files/2020/10/2540175_ZbtXBdFgQUWJVZsD.mp4