"Naitwa Goodluck Loth Mwakisiala, ni mkazi wa King’azi A.
Sisi huku kwetu tumevamiwa usiku wa jana na watu ambao wanasadikiwa kuwa ni askari, lakini sisi hatuna taarifa na ujio wa hao askari. Alafu askari wamekuja usiku wa manane. Na sisi sio vibaka wala sio wezi, ni raia wa kawaida.
Na kama askari wanaona sisi tuna makosa, wanapaswa kututumia barua za wito ili sisi twende, kwa sababu sio wahalifu. Na kitu kingine, kama sio kututumia barua za wito, basi waje kutukamata ikiwa ni mchana kweupe.
Nchi yetu tunafahamu kwamba kuna matukio ya utekaji. Sasa wanakuja usiku wa manane kuja kutuvunjia milango ili watuchukue, na mimi nilikimbia nilipoona sielewi. Hakuna taarifa ya mjumbe, wala hakuna taarifa ya mtu yeyote kuja nyumbani kwangu.
Kwa hiyo, huu uharibifu, hawa askari ambao wanasema wanalinda usalama wa raia na mali zao, hivi ndivyo walivyofanikiwa usiku wa jana kulinda usalama wangu na mali zangu. Na hizi ndo mali zangu kama mnavyona.
Na hapa nyumbani, wamemchukua mke wangu na hapa ndani nilikuwa na mgeni wangu ambaye alikuja nyumbani naye wambeba, ambaye hajui chochote kinachoendelea.
Na masuala mazito ambayo yanapelekea jambo ni uvamizi wa ardhi. Wamekuja kutuvamia kwenye hizi ardhi wakimkabidhi mtu mwingine kwamba ni ardhi yake, na hii sio ardhi yake. Na hawa watu wanatumwa na DC Magoti, ndiye anayewatuma huko, amewapa mamlaka ya kuja kutusumbua sisi wananchi. Na kila siku Defenders zinamaliza mafuta ya serikali kuja kutusumbua sisi wananchi. Wanakuja kutusumbua kila siku hatulali.
Sasa, sauti hizi tunazipaza sisi wananchi ili popote pale walipo viongozi ambao wanaweza kutatua changamoto yetu, waweze kutusaidia kwa sababu kama Mkuu wa Wilaya anaweza kutufanyia kitu kama hiki, sisi tutakimbilia wapi isipokuwa kwenu?
Na sisi tunataka kujenga uaminifu kwa serikali kwamba serikali inajali raia wake na sisi ni raia. Ili sisi tuipende serikali ni lazima serikali ifanye ushawishi kwetu sisi, kwa mfano kutulinda sisi pamoja na mali zetu, kutulinda na haya matukio ya uvamizi wa maeneo ambayo hatuelewi mwisho wake ni upi. Kikundi cha watu wachache ambao wanajiona wana hela kuliko wenzao wanakuja kutusumbua sisi wananchi."