Man, unalinganisha vitu visivyolingana, sisi bado tunapambana hata na mlo tu kwa siku achilia mbali maji masafi ya kunywa au umeme.
Hao hawakufikia hapo kwa kupenda, hiyo ni jamii inayofwata fairness na siyo ujinga wa akina Mwigulu na Nape, kila mtu Japan anaweza kuwa na maisha yake na kazi yake hahitaji msaada wa ndugu, wewe unasema hivyo Tanzania kwa sababu unaishi na kulea watoto wa mjomba, shangazi, kaka au sijui housegirl aliyekuachia na kukimbia ndiyo maana kila siku una watu nyumbani wa kutuma hapa na pale na iko hivyo kwa sababu Tanzania ni jamii ya dhulma, raisi mstaafu ana majumba yake tayari bado anajengewa nyumba na serikali, ukihoji unajibiwa kwa kejeli acha wivu.
Hapo walipofikia Wajapani ni maendeleo na watatafuta suluhisho lkn bado huwezi waambia waje kuishi maisha ya dhuluma na kunyonyana kama Tanzania, Makamba anakata umeme masaa 16 kwa siku bila ya consequence yoyote ile kama Waziri mwenye dhamana, watu hawawezi kufanya kazi kujiingizia kipato lkn yeye anacheka tu na kuwakebehi hao Wajapani walipambana wakatoka huko, sasa maendeleo na fairness kuna gharama yake …