POTOSHI Video ya Askari polisi akilia kwa uchungu baada ya Mkewe kuuliwa na watu wasiojulikana

POTOSHI Video ya Askari polisi akilia kwa uchungu baada ya Mkewe kuuliwa na watu wasiojulikana

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Kuna hii video inamuonyesha moja ya mtu ambaye inasemekana ni Askari polisi akilia sana na kwa uchungu baada ya mke wake kuuwawa na watu wasiojulikana.

Na moja ya kauli yake anasema ninawalinda watu ila mimi nimeshindwa kumlinda mke wangu hadi kauwawa

Je hii video upi uhalisia wake ni ya lini

​
1771918840331.png

 
Tunachokijua
Kumekuwepo na kipande cha video kinachomuonesha mwanaume mmoja akilia kutokana na kifo cha mkewe na kuelezwa kuwa mwanaume huyo ni Askari Polisi.

Uhalisia wa video hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa Taarifa hiyo ni Potoshi.

Kupitia nyenzo za kidigitali ikiwemo utafutaji wa maneno muhimu pamoja google reverse image search imebainika kuwa video hiyo imekuwepo mtandaoni angalau kuanzia Feb 13, 2023.

Taarifa pamoja na video hiyo inamuhusu mwanaume mmoja mkazi wa Kagera ambaye kwa kipindi hiko alikuwa ni Mwenyekiti wa mtaa wa National Housing kata ya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba ambaye alilamika kuuliwa kwa mkewe.

Taarifa ya Polisi iliyotolewa na kamanda wa polisi wa mkoa ilieleza kuwa Khadija Ismail (29) alibakwa na kuuliwa kwa akupigwa na kitu butu kichwani na mwanaume mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Paschal Kagwa.
Back
Top Bottom