- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Instagram, likidai kuwa Hashim Rungwe amefichua siri kwamba viongozi wa vyama vya siasa walilipwa fedha ili kushiriki kikao kilichoitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan.
Chapisho hilo limeambatanishwa na kipande cha video kilichokatwa, kinachomuonesha Hashim Rungwe akizungumza katika kipindi cha Medani za Siasa kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star TV.
Chapisho hilo lilianza kusambazwa mara baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya kikao maalumu na viongozi wa vyama vya siasa nchini kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Hata hivyo, ufuatiliaji uliofanywa kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya mtandaoni umebaini kuwa baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Hashim Rungwe hakufanya mahojiano na chombo chochote cha habari akidai kuwa yeye au viongozi wengine walilipwa na Serikali ili kushiriki kikao hicho.
Uchunguzi zaidi umeonesha kuwa video iliyotumika kwenye chapisho hilo si ya tukio la hivi karibuni. Badala yake, ni sehemu ya mahojiano aliyoyafanya Hashim Rungwe katika kipindi cha Medani za Siasa cha Star TV, ambayo yamekatwa na kutumika nje ya muktadha wake ili kuhusishwa na kikao cha hivi karibuni cha Rais Samia na viongozi wa vyama vya siasa.
Aidha, chapisho hilo lililochapishwa na ukurasa unaojulikana kama Chief Odemba liliambatana na nukuu isemayo:
"Kila tukienda kwenye mikutano tunapewa pesa na CCM ili ionekane nchi hii kuna demokrasia. Hospitalini hakuna dawa, lakini pesa za kutulipa wanapata, na sisi hatutaacha kuzichukua."
Hata hivyo, hakuna ushahidi unaoonesha kuwa Hashim Rungwe ametoa kauli hiyo kuhusiana na kikao cha Ikulu. Badala yake, chapisho hilo limetumia video ya zamani na kuiwasilisha kana kwamba inahusu tukio la sasa, jambo linalopotosha umma.