Video ya kusikitisha ya Rah P Akielezea Alivyoteswa na Kuzalishwa Watoto Wawili Marekani

Video ya kusikitisha ya Rah P Akielezea Alivyoteswa na Kuzalishwa Watoto Wawili Marekani

Yuko poa lakin ,mambo ya chura,meno yake na ameonesha yeye kweli ni mwanamke,ana swagga,amelia.yuko poaa
Mkuu umeongea kitu kikubwa sana....
AMELIA..... Mwanamke anapolia japo moyo wake unakuwa kwenye maumivu makali ila hiyo kwa sisi mabazazi inakuwa inatupa kitu flan hivi....
 
Mi sidhan kama kuna ktu cha kujutia, inshort huko USA atakua kajifunza vitu vingi sana na kapata exposure ya kutosha so atumie hyo experience kuendeleza maisha yake hapa bongo au popote, hata angekua bongo pia yangemkuta tu, cha msingi ni kuendelea kukimbiza ndoto zake
 
Tuongee ukweli, pamoja na yote, Life lake na life la wadada wa kibongo walio kwama, kama sista P, zay b na wengine wengi. wapi linawapiga zaidi? Rap P apartment kali, gari safi, ngozi inawaka, yaani kila kitu utamu. Bora akae uko uko maana angekuwa bongo pengine angekuwa kama Madame uchwara
Yes hata Mimi nimeona hana shida sana au pengine alikua Ana expect makubwa zaidi, but hata changamoto alizopata huko ni elimu tosha, elimu sio lazima ukae darasani
 
Mi naona kama anatafuta kick tu! kusupport track yake! Muuza unga for years mke wake lazima ajue kutokana na nature ya biashara yenyewe. kuna ka ukweli hakasemi! sababu siri yake...
 
mbona miaka yote ameishi nae poa tuu japo kuwa ni drugdealler,ndo maana wana fasihi wanasema,usipende xn kuupekua ukwel maana huwa unauma
 
Kwa muda mrefu rapper wa kike aliyewahi kutikisa nchini Tanzania, Rah P amekuwa kimya na kuendelea na maisha yake nchini Marekani.

Lakini wengi hawajui tabu na shida alizozipata baada ya kwenda nchini humo kutafuta maisha na kufuata ndoto yake. Hii ni interview iliyofanywa na Kali TV Online ambapo anasimulia jinsi alivyohangaika baada ya kuzalishwa watoto wawili na mwanaume ambaye alikuja kugundua kuwa ni muuzaji wa madawa ya kulevya.

Baadaye mwanaume huyo alikuja kukamatwa na hivyo kubaki mwenyewe akiwahudumia watoto wake wakati hakuwa na kazi. Baada ya hali hiyo alijikuta katika wakati mgumu na kusongwa na mawazo mengi kiasi cha kumfanya awe mlevi na kujikuta akifungwa jela.

Sasa anataka kufufua tena ndoto yake ya kufanikiwa kimuziki nchini Marekani. Atafanikiwa akiwa tayari ni mama wa watoto wawili?
 
Back
Top Bottom