POTOSHI Video ya Museven akifanya mazoezi ya kila siku akiwa ikulu

POTOSHI Video ya Museven akifanya mazoezi ya kila siku akiwa ikulu

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
MUSEVEN.jpg

 
Tunachokijua
Yoweri kaguta Museveni ni mwanasiasa, na Rais wa sasa wa Uganda ambaye amekuwa madarakani tangu Januari 26, 1986. Katika uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwaka wa 2026, alishinda tena na kuingia katika muhula wake wa saba wa uongozi.

Madai

kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na video ambayo imechapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya facebook ikidaiwa kumuonesha rais wa Uganda Yoweri kaguta museven akiwa kwenye mazoezi yake ya kila siku

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao umebaini kuwa video hiyo ni ya zamani,ambayo ilirekodiwa Aprili 9, 2020, wakati wa janga la ugonjwa wa COVID-19.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari, video hiyo ilimuonesha Museveni, aliyekuwa na umri wa miaka 75 wakati huo, akikimbia ndani ya ofisi yake na kufanya mazoezi ya kusukuma mwili kwa mikono (push-ups).

Video hiyo ilitolewa katika kipindi ambacho Uganda ilikuwa imeweka vizuizi vya shughuli za umma kutokana na janga la COVID-19.

Museveni alitumia video hiyo kuhamasisha wananchi kuendelea kufanya mazoezi wakiwa majumbani ili kulinda afya zao wakati wa kipindi hicho.
Back
Top Bottom