Mtanganyika...
Hiyo video Nyerere yuko Lindi ni mwaka wa 1959.
Unauliza gari hilo kwenye hadithi yangu inapatikana ukurasa wa ngapi.
Kwenye toleo la kwanza la kitabu cha Abdul Sykes, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," (London 1998), hadithi hii iko uk. wa 197.
Ni kisa cha kusisimua cha Ali Mnjale na Salum Mpunga waliokuja kuhudhuria mkutano wa kwanza wa TANU mwaka wa 1955 uliofanyika Ghadhi Hall Dar-es-Salaam.
Baada ya mkutano wajumbe hawa walikutana na uongozi wa TANU New Street kufahamisha tatizo lililoko Southern Province ambako makao yake makuu ni Lindi.
Huko Kusini kanisa lilikuwa linawatisha waumini wake wasijiunge na TANU kudai uhuru wakiwaambia kuwa Waislam walikuwa wanajipanga upya kuanzisha Maji Maji nyingine.
Ujumbe ule ukamtaka Mwalimu Nyerere aende Kusini kuzungumza na wananchi kuhusu nia na makusudi ya TANU.
Mwalimu alikwenda Lindi akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Yapo mengi lakini tusimame hapa kwa sasa.
Wakati huo hao wenye hilo gari walikuwapo lakini hawakuwa karibu ya Nyerere kama alivyokuwa Sheikh Yusuf Badi, Ali Mnjale, Suleiman Mnonji, Mussa Athmani Lukundu, Yusuf Chembera kwa kuwataja wachache.
Hao wenye gari walisubiri hadi mwaka 1959 ndipo walipojitokeza kupiga picha na Nyerere.
View attachment 1956568