Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Video inayoonesha wasichana wa shule wakiwa wamejipanga msururu kwa ajili ya kunyunyiziwa dawa kama sehemu ya hatua za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona imeleta mgawanyiko miongoni mwa Wakenya mtandaoni.
Video fupi ya sekunde 30 iliyopakuliwa kwenye Twitter na gazeti nchini humno inaonesha mwanaume aliyevalia mavazi ya kujikinga akiwanyunyizia kimiminika wasichana kwenye mikono, miguu na sare za shule:
Shirika la afya duniani halishauri kuwanyunyizia watu dawa ya kuua virusi na linasema inaweza kuleta madhara ‘’kimwili, na kisaikolojia’’
Shule zimefunguliwa Jumatatu nchini Kenya kwa ajili ya wanafunzi wanaohitimu huku miongozo ikitolewa kuhusu utoaji wa vitakasa mikono na mahala pa kunawa mikono na kuzingatiwa kwa sharti la kutosogeleana ili kuzuwia usambaaji wa virusi vya corona.
Wakenya kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wameelezea maoni yao tofauti kuhusu kunyunyiziwa kwa wanafunzi.
"Vitu kama hivyo na vifaa vya kunyunyiza vilipigwa marufuku na wizara ya afya Kwa vipi watu wazima wanakaa chini na kuamua kwamba kuwanyunyizia watoto kama hivi kutadhibiti #Covid19? Vipi kuhusu maji na sabuni ? " Dkt Mercy korir aliandika kwenye tweeter.
"Halafu kuanzia siku inayofuata tunakua na matatizo ya ngozi, kifua,maradhi ya pumu yote kwa sababu ya kisingizio cha pesa. Wazazi walilazimika kulipakwa ajili ya watoto wao ili wanyunyiziwe dawa kama ng’ombe ,"Phill Kamara aliandika tweeter.
"Sioni tatizo lolote kuhusu shughuli hii.. Ulitarajiwa watatakaswa vipi na maambukizi? .. Baadhi yenu ni waasi tu bila sababu," Denno Duevshi aliandika mtandaoni.