SI KWELI video ya watu wakikanda chapati kwa miguu ni halisi?

SI KWELI video ya watu wakikanda chapati kwa miguu ni halisi?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kumekuwepo na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Instagram na Facebook, ikionyesha baadhi ya watu wakidaiwa kuandaa chapati kwa kutumia miguu. Katika video hiyo, watu hao wanaonekana wakikanda unga wa ngano kwa kutumia miguu yao.

Moani ya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamesema kuwa hivi sasa wamefikiwa kwa wale ambao hawapendi kupika huku wakihamasishab kupika

Hata hivyo, kwa kutumia mbinu za ufuatiliaji na uchambuzi wa kidijitali, imebainika kuwa video hiyo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde

Katika mazingira ya kawaida , kukanda unga kwa kutumia miguu kunaweza kusababisha uharibifu wa chakula kutokana na uwezekano wa kuhamisha vijidudu kutoka kwenye ngozi na mazingira kwenda kwenye unga.

Miguu huwa katika hatari kubwa ya kukusanya bakteria, fangasi, uchafu na jasho kutokana na kugusana mara kwa mara na sakafu, viatu

Katika usalama wa chakula, maandalizi ya chakula yanapaswa kufanyika kwa kutumia mikono iliyosafishwa vizuri au vifaa safi vinavyofaa kwa ajili ya kuchanganya na kukanda unga . Hii husaidia kupunguza uwezekano wa bakteria na uchafu mwingine kuingia kwenye chakula.

Video imechapishwa sehemu kadha wa kadha ikwemo hapa ,hapa, hapa, hapa, hapa hapa
CHAPATI.jpg

 
Hivi mpaka sasa watu bado hawajajua kutofautisha picha halisi na za AI? Hii hata mtoto wa baby class anajua ni AI.
 
Back
Top Bottom