SI KWELI PreGE2025 Video yenye picha na Sauti ya Heche akiongea kuhusu Lissu

SI KWELI PreGE2025 Video yenye picha na Sauti ya Heche akiongea kuhusu Lissu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Kuna hii video inasambaa TikTok ikiwa na picha ya makamu mwenyekit CHADEMA akiongea kuhusu Lissu je ni sauti ya HECHE au ni wapotoshaji?
1754890853508.png
 
Tunachokijua
John Heche ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Taifa wakati Tundu Lissu ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa.

Madai

Kupitia mtandao wa Tiktok mtumiaji mmoja amechapisha ujumbe ulioambatana na sauti inayoaiwa kuwa ni ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche akimlaumu Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu ambaye yupo gerezani kwa sasa.

Uhalisia wa sauti hiyo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa sauti hiyo ni ya kughushi.

Ufuatiliaji kwa njia ya nyenzo za kidigitali umejiridhisha kuwa sauti hiyo si ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche na badala yake imeigiliziwa na mtu tofauti.

Sauti hiyo inayosikika inaonekana kuwa ni ya kujilazimisha kutokana na kuvuta maneno, mawimbi ya sauti, namna ya utamkaji wa maneno na kupanda na kshukwa kwa sauti hiyo si halisi ukilinginisha na sauti halisi ya Heche.

Kutokana na hali inayoendelea ndani ya chama hicho ukilinganisha na maneno yanayotamkwa kwenye video hiyo inaonesha kwa kiwango kikubwa ni maneno ya kutengenezwa ambayo yanakinzana kwa kiwango kikubwa na maneno ambayo Heche amewahi kuyatamka mara kadhaa hadharani.
Ni yeye kabisa huyo! Kaongea yaliyo ndani ya moyo wake, Lisu kaharibu Chadema kweli. Tumempoteza Lisu, tumepoteza luzuku, tumepoteza chama, tumepoteza wanachama (in Heche's voice)
 
Ni yeye kabisa huyo! Kaongea yaliyo ndani ya moyo wake, Lisu kaharibu Chadema kweli. Tumempoteza Lisu, tumepoteza luzuku, tumepoteza chama, tumepoteza wanachama (in Heche's voice)
nakuona mkereketwa'
 
Ni yeye kabisa huyo! Kaongea yaliyo ndani ya moyo wake, Lisu kaharibu Chadema kweli. Tumempoteza Lisu, tumepoteza luzuku, tumepoteza chama, tumepoteza wanachama (in Heche's voice)
Arud twishen akajifunze nafikiri itachukua miaka 3 mpk kuipatia sauti
 
Back
Top Bottom