Video za uokozi maafa ya kariakoo

Video za uokozi maafa ya kariakoo

IMG-20241118-WA0028.jpg
 

Je, fedha za bajeti ya maafa zinafanya kazi gani? Kwa nini wasichote huko na kuzitumia katika janga hili?
Kama bajeti ya maafa haipo, Je, kwa nini wasipitishe bajeti ya dharula ili kupata fedha za kuhudumia kwenye janga hili!

Je, Serikali inataka kuligeuza janga hili kama chanzo cha mapato kama ilivyokuwa kwa janga la tetemeko la Ardhi kule Bukoba????
 
Kila mtu kwenye haya maisha ana umuhimu wake, ni suala la muda tu umuhimu wa mtu kuonekana. Leo, walewale machinga, tunaowaita wazururaji, ndio wameokoa watu wengi zaidi kuliko wale tunaowalipa mishahara. Kila mtu aheshimiwe, apewe thamani anayostahili na tutumie busara juu yao.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa miili 13 ya waliothibishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufariki baada ya ghorofa kuporomoka Kariakoo itaagwa katika Uwanja wa Mnazi Mmoja kuanzia saa 7 mchana mpaka saa 10 jioni.

Akizungumza na wanahabari usiku wa kuamkia Jumatatu Novemba 18, 2024 , RC Chalamila amesema kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ndiye atakayeongoza zoezi la kuaga miili hiyo, huku akiwaalika watu wote walioguswa na msiba huo kuhudhuria kutoa heshima za mwisho kwa marehemu wote.

"Inawezekana ratiba hii imekuwa ya haraka lakini ni kwasababu ya maombi ambayo yamefanywa na baadhi ya ndugu wa marehemu na kutokana pia na ushauri wa kitabibu uliotolewa na madaktari kuhusiana na namna tunavyoweza kuikabidhi miili hii kwa wenzetu wapendwa ambao wanatamani sasa kuwasindikiza marehemu", ameeleza Chalamila.

Aidha amesema kuwa ndugu wote wa marehemu wanatakiwa kufika Hospitali ya Amana saa mbili kamili asubuhi ambapo watakutana na Mganga Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kupewa utaratibu wote wa kukabidhiwa miili ya ndugu zao.

Hata hivyo RC Chalamila amewatoa hofu wananchi kuwa zoezi la kuaga marehemu halitasitisha uokoaji ambao bado unaendelea katika jengo hilo lililoporomoka kama ikibainika bado kuna watu waliokwama ndani.
20241118_145002.jpg
 
#UPDATES Wakati zoezi la kutoa misaada mbalimbali likiendelea Kariakoo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na Uratibu. Dkt. Jim James Yonazi amewataka wananchi kuwa makini kuhusu michango inayoendeshwa ya kuwasaidia wahanga ambapo ameweka wazi kuwa akaunti inayokusanya michango ya fedha ni moja pekee na sio nyingine.

Dkt. Jim James amesema michango yote inayohusu tukio hilo inakwenda kwenye akaunti maalum ambayo ni ya serikali #EastAfrica
20241118_151240.jpg
TV
 
Kijana Seba aliyeandika message kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho siku mbili zilizopita.

1732254002610.jpg



Mwili wake umeopolewa mda huu ukiwa tayari umeshaanza kuaribika kwenye jengo la Kariakoo.. Tayari mwili wake umepelekwa kwenye hospitali ya Amana kwa kwa taratibu nyingine za kuhustili..Roho ya marehemu ipumzike mahara pema peponi 😭😭 Inasikitisha sana jamani Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un💔🙏
downloadfile-2.jpg
 
 
Back
Top Bottom