VIDEO: Zamaradi aonyesha White house yake na mume wake

Katika vitu ambayo sivipendi basi ni kuishi na mifugo ndani ya nyumba [emoji51]
 
Ngoja bavicha waje
 
Katika vitu ambayo sivipendi basi ni kuishi na mifugo ndani ya nyumba [emoji51]
Ndio maana nikasema kila mtu na mapenzi yake. Alafu kufuga ndani ya nyumba ni tabia. Ww Jaribu siku kumuoa msichana aliyekulia mitaa ya uswahilini uone kama hata utaweza kufuga Ktk maisha yako.
 
beautiful house. Hongera sana kwa mmiliki.
 
Nyumba nzuri ila mbwembwe za maswiming pool ya nini.? Piga banda la kuku walau wa kula nyumbani na wa kujifunzia ujasiriamali watoto. Au unapiga bustani ya maua/mbogamboga.

Amejitahidi Zamaradi na mume wake


Mkuu siyo kila mtu anawaza kufuga au kulima bustani ya mboga au kufanya biashara. Unajuaje kama hana hiyo bustani sehemu nyingine?? Unajua wewe mawazo yako yana-reflect uwezo wako wa kiuchumi. Ndo maana unaona swimming pool ni mbembwe. Wallah ungekuwa na uwezo hata mawazo yako kwenye hili bandiko yangekuwa tofauti. Hauna tofauti na yule anayeendesha Vitz akiona mwenzake anasukuma BMW au VW anajifariji kwamba wote wana magari! Deep down reality anaijua. Ukitaka kuishi vizuri....daima kubali hali yako. Na wale waliokuzidi kipato wapongeze kwa mafanikio yao.

Haya maisha hayataki hasira Mkuu. Pambana na hali yako.
 
Hahahaaa.. Umeni judge kwa comment yangu. Niliyotoa ni maoni yangu na ni kama priorities zangu nikiwa kwangu na nilifundishwa toka niko young. Sasa wewe ukaamua kunikosoa ukavuka na mipaka ukaamua kunijudge..!! Its ok na wewe umetoa maoni yako.[emoji122] [emoji122]
 
Barakah da prince alifanya nini mkuu tujuze.??
Wasanii bwana kila kitu wao Acting hata sehemu hisiyohitaji Acting,kuna kosa ukisema hauna nyumba? Prince bado mdogo asishindane na kina mond kuna Mambo mengi behind fedha za watu.
Aliitangaza nyumba ya mama mkwe wake kwamba yake badae akaja kuumbuliwa na shemeji yake
 

Samahani bro. Sijakujaji na wala hilo halikuwa lengo langu. Nilitaka tuu kuonyesha kwamba kuweka swimming pool siyo mbwembwe. Again kila mtu ana priorities zake kama ulivyosema.

Apologies kama nimekukwaza Kiongozi. Pamoja sana!
 
Yule mtangazaji wa clouds fm aliekua na mke wa boss wa clouds ameonysha mjengo wake ambao haujakamilika akiuita small whitehouse, ikiwa half court ya basketball na swimming pool likiwa linajengwa. Big up kwake
Nani kakuambia hiyo nyumba ni ya zamaradi?
 
Uchafu umekuwa sehemu iliyokubalika ya utamaduni wetu kiasi kwamba hata mtu anapotaka kupiga picha ya kuonesha dunia nzima nyumba yake, hajali hata kufanya usafi kidogo tu.

Hapo nje makorokoro hayo yamekubalika kabisa kwamba ni poa tu yawepo hapo kama sehemu ya asili ya nyumba hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…