Mkuu siyo kila mtu anawaza kufuga au kulima bustani ya mboga au kufanya biashara. Unajuaje kama hana hiyo bustani sehemu nyingine?? Unajua wewe mawazo yako yana-reflect uwezo wako wa kiuchumi. Ndo maana unaona swimming pool ni mbembwe. Wallah ungekuwa na uwezo hata mawazo yako kwenye hili bandiko yangekuwa tofauti. Hauna tofauti na yule anayeendesha Vitz akiona mwenzake anasukuma BMW au VW anajifariji kwamba wote wana magari! Deep down reality anaijua. Ukitaka kuishi vizuri....daima kubali hali yako. Na wale waliokuzidi kipato wapongeze kwa mafanikio yao.
Haya maisha hayataki hasira Mkuu. Pambana na hali yako.