Vidokezo vya ulaji bora na vyakula vya kuepukwa kiafya

Vidokezo vya ulaji bora na vyakula vya kuepukwa kiafya

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Mafuta-mengi-798x350.jpg


KATIKA maisha, mwanadamu anapitia awamu mbalimbali za maisha. Kila awamu ya maisha inahitaji ulaji wa chakula cha aina yake. Mwili wa mtoto unahitaji virutubishi ili kusaidia ukuaji wa mwili. Mwili wa kijana una mahitaji maalum kwa ajili ya kudhamini ukuaji wa kiafya, wakati mtu mzima anahitaji chakula cha kulinda mwili ili uzito wake uende sambamba na mwili wake.


Lakini pia kuna mahitaji ya vyakula kwa makundi maalum. Kwa mfano, kina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha wana mahitaji yao ya vyakula tofauti na kina mama ambao hawako katika kundi hilo.


Baadhi ya tafiti za kitiba zimebainisha kwamba hali ya kiafya ya mama mjamzito huathiri pia mtoto aliyeko tumboni bado. Upo uhusiano, kwa mujibu wa tafiti hizo kwamba baadhi ya magonjwa sugu yanayowapata baadhi ya watu ukubwani, yaliwaanza wakati wakiwa bado tumboni mwa mama zao.


Kwa hiyo, ni muhimu kwa kina mama wajawazito kuzingatia ulaji wa vyakula mara tu baada ya kushika mimba kwa sababu ulaji bora, unafaida nyingi mwilini mwa mama mjamzito, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa kinga mwilini na kufanya mwili kupambana kirahisi na maradhi mbalimbali, kujenga siha nzuri (afya bora), kuleta furaha na amani, kusaidia ukuaji wa mwili na akili, kuleta nguvu na kusaidia mwili kufanya kazi vizuri.

Soma zaidi makala hii:
http://www.fikrapevu.com/vidokezo-vya-ulaji-bora-na-vyakula-vya-kuepukwa-kiafya/
 
Back
Top Bottom