Sio rahisi kupata msaada hapa kwa sababu maelezo yako hayatoshelezi. Nimeona umegusia issue ya wanao kuwashwa na kama wenzangu hapo juu walivyosema, huo ni ugonjwa wa scabies, japo nasita kusema ni scabies kwa sababu scabies haina vidonda kama vidonda, bali mtu hupata upele wenye uvimbe unaowasha.
Kama ni scabies, basi hizo ni parasites, na kawaida mtu huwa anawashwa sehemu walipoingilia. Kama dudu lako linawasha, nasikitika kwamba uliipata kwa njia ya ngono, na inawezekana wewe ndiye uliyeambukiza watoto kwa kuwagusa. Kama ni mara ya kwanza kuugua Scabies, maana yake hawa parasites wanaweza wakakaa kwenye mwili wako hadi mwezi kabla ya kuanza kuwashwa. Mara nyingi muwasho wa scabies huwa ni maradufu mida ya usiku.
Kama hujaipata kwa njia ya ngono basi mazingira ya hapo home kwako sio mazuri, maana yake ni pachafu.
Parasites wanaosababisha scabies ni wagumu kufa kwa sababu wana mayai mengi na mayai yao yana tabia ya kutulia mpaka wahisi kuna chakula ndiyo wajitokeze.
Kama una scabies kweli na familia pia wanawashwa, tafuta dawa ya kumeza inaitwa Ivermectin nadhani kidonge ni 8,000 na wanauza kutokana na uzito. Unaweza ukaambiwa utumie vidonge 6 au 7. Sasa hapo inabidi ununue kwa familia nzima lakini usiwape watoto chini ya miaka mitano. Lakini pia kuna dawa ya kupaka inayoitwa scaborma au Eurax Kwa maana hiyo unatumia vidonge na cream ya kupaka.
Kama hali sio nzuri kifedha, basi nunua mafuta ya nazi pamoja na mafuta ya mwarobaini. Changanya kwa ratio ya 0.5 kwa 1. Paka asubuhi na usiku baada ya kuoga wewe na familia nzima mpaka muwasho uishe kabisa na ikibidi endelea kupaka. Itabidi uvumilie harufu.
Unapokuwa unatumia dawa za scabies au mafuta ya mwarobaini, hakikisha mnafua mashuka na nguo zote na kuzianika juani. Usivae nguo uliyofua haraka. Fungia kwenye mfuko wa nailoni nguo au mashuka uliyoyafua na kukauka kwa siku saba ili wale parasites wafe kwa kukosa hewa. Hakikisha nguo zinachomwa na jua kisawasawa.