Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mwanamke mmoja wa Vietnam mfanyabiashara tajiri wa kutupwa anefanya biashara ya kuuza nyumba na majengo (Estate and property Developer) amehukumiwa kifo baada ya kupiga fedha kiasi cha dola bilioni 12.5
Katika kesi kubwa ya ufisadi na upigaji ilomkabili mwanamke huyo Truong My Lan, imedaiwa kuwa kati ya mwaka 2012 na 2022 mwanamke huyo akitumia kampuni yake ya Van Thinh Phat aliweza kuidhibiti benki moja ya Saigon Joint Stock Commercial Bank na kupitisha fedha za upigaji kwenda kwenye akaunti hewa zenye makampuni hewa.
Pia wakati huohuo inadaiwa Truong alikuwa akificha uhalifu wake kwa kuwalipa na kuwaziba midomo maofisa mbalimbali wa serikali ili wasifichue upigaji wake.
Wachunguzi na wachambuzi mbalimbali duniani ambao wamevutiwa na kuanza kudadisi kuhusu kesi hiyo ya aina yake wamekuwa wakijadili ni njia zipi mama huyo Truang alikuwa akitumia kuwa miaka kumi bila kugundulika?
Vikampuni hewa.
Lakini wachunguzi nchini Vietnam walibaini kuwa mama huyo kwa kutumia kampuni yake ya Van Thinh Phat aliweza kufungua vikampuni vidogovidogo vipatavyo 1000 ambapo aliweza kutumia majina ya vikampuni hivyo kuomba mikopo katika mabenki nchini Vietnam hususan benki ya SCB.
Kwa mujibu wa televisheni ya serikali ya VN Express mikopo hiyo ilolipwa kwa vijikampuni hivyo imeisababishia serikali hasara ya dola bilioni 27.
Katika kujiweka sawa kifedha pia Truong aliweza kufanikisha uuzwaji wa benki ya Saigon ilonunuliwa na benki ingine ya SCB katika mchakato wa kipigaji ulosimamiwa na benki kuu ya Vietnam ambapo maofisa wanosimamia huduma za kibenki walilipwa ujira wa fedha.
Mmoja wa lmaofisa hao wa benki ambae alilipwa Truong fedha kaisi cha dola milioni 5.2 tayari yupo jela akitumikia kifungo cha maisha kwa kufanikisha upigaji huo pamoja na kukiuka taratibu za kibenki au twasema "violating banking regulations".
Kashfa ilomfanya raisi ajiuzulu.
Mapema mwaka 2023 raisi Nguyen Xuan Phuc alikumbwa na kashfa ya ufisadi na upigaji ambapo wakati wa kipindi cha ugonjwa wa uviko -19 aliruhusu ipigaji kutamalaki. Raisi Nguyen alipatwa na kashfa hiyo baada ya kampeni ya kupambana na ufisadi iloanzishwa na katibu mkuu wa chama tawala cha kikomunisti, kushika kasi.
Katibu mkuu wa chama cha kikomunisti Nguyen Phu Trong alianzisha kampeni ya kupambana na ufisadi mwaka 2016 iloitwa "Blazing Farnaces" ambapo alisema nchi bila kuw ana nidhamu kutakuwa an vurugu na ghasia na hivyo kulihitajika uwiano kati ya demokrasia na utawala wa sheria.
Katika kuthibitisha kuwa kampeni hiyo ya "Blazing Farnaces" ina nguvu, aliekuwa raisi Von van Thuong mwezi march mwaka huu alijiuzulu nafasi yake baada ya kugundulika kuwa nae ni mshiriki wa ufisadi na upigaji.
Katika kipindi cha miaka mitatu maraisi wawili wa Vietnam wamejiuzulu kwasababu ya kunyamazia ufisadi unofanywa na watu wa chini, maofisa wa serikali, mabenki pamoja na wafanyabiashara.
Kampeni iloanzishwa na bwana Trong yaonyesha yaweza kufanya kazi pale inaposimamiwa kikamilifu na viongozi badała ya kusitishwa au kufia njiani ambapo nchi inakuwa haiendelei au kutoona maendeleo yoyote ya kiuchumi.
Nao mfumo wa Kleptokrasia ambao hutumiwa na viongozi mafisadi inaonyesha kuwa waweza kudhibitiwa na kuondolewa pale tu umakini na ufuatiliaji unapopewa kipaumbele na kiongozi na timu yake badała ya kuuachia uote mizizi.
Vyanzo vilotumika: Reuters, VN Express. Corruption watch na AP.