mkuu yotube wanalipa hadi dola 5 ( 10,000/=) pesa ya madafu endapo channel yako ina watazamaji wa ulaya na marekani.
ila kwa views za huku africa youtube hulipa kwa wastani elfu 2 na ushehe kwa views elfu 1 (japo wapo wanapokea elf 5 kwa views buku kulingana na jampuni inayotaka itangaziwe matangazo yale ya youtube).
sasa kwa spidi ya views ya gii video najua wiki ikiisha views kama laki 3 hapo zimo, kwa views laki tatu hapo ukilipwa chini basi ni kama laki sita.
millard enzi hizo akipandisha tu hata video moja ya birthday ya shilole ana views nyingi tayari na alikuwa anapandisha videos kibao na zinahit, kijana hakuwa na mpinzani
View attachment 1439892
ila kama unadhani rahisi kufikisha hata views laki jaribu uone shughuli yake,
jii ni listi ya watu wanaolipwa zaidi na youtube, anaeshika mkia kwenye listi hii analiwa bilioni 30 *(30,000,000,000)
Usione korona ipo, hakuna shows ukadhani watu hawapigi pesa, msanii kama Diamond youtube inamrushiaga hela yake ya videos za gharama na anabakiwa na kitita cha maana tu