Vifaa 3 muhimu kwenye utengenezaji wa incubator ya kutotolesha mayai

Vifaa 3 muhimu kwenye utengenezaji wa incubator ya kutotolesha mayai

Joined
Sep 11, 2018
Posts
44
Reaction score
58

Brown and White Modern House for Sale Real Estate Facebook Post_20260926_162318_0000.png

UTENGENEZAJI WA INCUBATOR YA KUTOTOLESHA MAYAI​

Unapotengeneza homemade incubator, siyo tu kuweka bulb ya joto ndani ya boksi na kutegemea mayai yatotolewe. Mfumo wa kudhibiti joto na unyevu una nafasi kubwa kwenye matokeo ya utotoleshaji.

Kuna vifaa vitatu ambavyo vinaweza kufanya mfumo wa incubator uwe bora zaidi:

1️⃣ Temperature & Humidity Controller​


Hiki ndicho kifaa kinachotumika kudhibiti joto na unyevu kulingana na settings ulizoweka.


Controller kama XK-W1099 au STC-3028 n.k inaweza kutumika ku-control vifaa vya kuzalisha joto na kuzalisha unyevu kwenye incubator yako.


2️⃣ Humidifier​


Humidifier hutumika kuzalisha unyevu (humidity) ndani ya incubator.


Badala ya kutegemea bakuli au chombo ulichoweka maji ndani yake pekee, humidifier inaweza kusaidia kuongeza unyevu kwa haraka zaidi, hasa pale ambapo unatotolesha idadi kubwa ya mayai.


3️⃣ Heating Bulb 💡​


Bulb ndiyo chanzo cha joto kwenye baadhi ya homemade incubators.


kulifanya joto libaki kwenye kiwango kinachohitajika bila kupanda na kushuka Hapo ndipo temperature controller inapoingia kwenye mfumo.


Kwa ufupi:​


Controller → inadhibiti joto na unyevu
Humidifier → inazalisha unyevu
Heating bulb → inazalisha joto



Lakini bado kuna vitu vingine muhimu kama fan ya kusambaza hewa, ventilation, sensor position na turning system.


💬 Kwa wanaotengeneza incubator zenu wenyewe:

Ni kifaa gani kati ya hivi ambacho umewahi kupata changamoto nacho?

Na kwa uzoefu wako, ni kipi kinaathiri zaidi ufanisi wa homemade incubator—joto, humidity au circulation ya hewa?
Tushirikishane uzoefu.
 
Unauzaje controler hio? Ninazo mashine kuhwa but nataka kutengeneza moja ndogo kwa ajili ya mayai ya Bata, make hizi kubwa haziangui vizuri mayai ya Bata
 
Unauzaje controler hio? Ninazo mashine kuhwa but nataka kutengeneza moja ndogo kwa ajili ya mayai ya Bata, make hizi kubwa haziangui vizuri mayai ya Bata
Tuwasiliane kupitia 0657 923 089
Controller zipo kuanzia 20,000. 35,000 n.k
 
Back
Top Bottom