Vifaa muhimu kwenye hardware

Vifaa muhimu kwenye hardware

Habari wakuu

Samahani sana Mimi nina mtaji mdogo wa 5m
Ila nahitaji ni fungue hardware itakayo kuwa na vifaa vidogo vidogo vitakavyo endana na bajeti yangu

Naomba kama kuna mtu yoyote mwenye list ya vifaa vya hardware anitumie ili inisaidie kufanya tathimini

Lengo ni kuanza na bajeti ya 5m, kama kuna mtu aliwahi kuanza na mtaji mdogo kama huu naomba anisaidie mawazo
Asanteni.
Hela yote nunua cement ndio iwe biashara yako komaa nayo ,endelea na cement mpaka mtaji wa 50 million kisha unauza cement na nondo za aina zote unapiga kazi mpaka ufike 100 unaweka cement ,nondo ,gypsam ,bati na vifungashio vyao.Nina hardware chukua ushauri ni bure.
 
Kwa mtaji huo ukianzisha hiyo ''biashara'' halafu ikifeli unaweza kukimbilia kwa mganga kuwa umelogwa? Mambo mengine ni kujitakia stress tu.
Siyo kweli, kuna jamaa alianza na milioni 3 tuu kijiduka kidogoo but now more than 20 milioni...
 
Hapana sio kweli usimkatishe tamaa iyo pesa ni nyingi sana inategemea yupo mkoa gani upatikanaji wa bidhaa upoje pia anaweza akaanza na cement,misumari pmj na nondo2 naakapiga kazi
Haya ni mawazo yako. Mimi sikumkatisha tamaa ila nimemwambia kulingana na uzoefu wangu. Najua jamaa zangu walioanzisha na mtaji mdogo waka-fail kwa sababu ya mtaji. Uamuzi ni wake na sijamlazimisha kufuata maoni yangu. BTW biashara kufanikiwa kwake siyo ukubwa wa mtaji bali ni uchapakazi, ujuzi na uzoefu wa mfanyabiashara kwenye eneo husika. Lakini mtaji unapokuwa mdogo, na pia hata hajui aanze na bidhaa gani huoni kama ni shida?
 
Kwa mil hizo anza na vifaa vya umeme na vifaa vya bomba. Vingi ni vidogo vidogo na kwa bei ya jumla utapata vingi na utokaji wake ni wa uhakika. Vingine utaongeza kulingana na eneo ulipo
 
Hela yote nunua cement ndio iwe biashara yako komaa nayo ,endelea na cement mpaka mtaji wa 50 million kisha unauza cement na nondo za aina zote unapiga kazi mpaka ufike 100 unaweka cement ,nondo ,gypsam ,bati na vifungashio vyao.Nina hardware chukua ushauri ni bure.
Huu ni ushauri bora sana Asante sana mkuu hapa nitajua nianze kuchekecha vipi ntakutafuta kwa ushauri zaidi
 
Kwa mtaji huo ukianzisha hiyo ''biashara'' halafu ikifeli unaweza kukimbilia kwa mganga kuwa umelogwa? Mambo mengine ni kujitakia stress tu.
Daah aisee kwa hiyo ukiwa na mtaji mkubwa ndio uhakika wa kufanikiwa? Hardware na wauzaji wa mbao wengi wameanza na mtaji mdogo na wamefanikiwa wengine wanapewa mali kauli tuu 5 m unaiona ndogo kwenye Biashara?
 
Mtaji mkubwa siyo uhakika wa kufanikiwa hata kidogo na wala mtaji mdogo siyo kufeli. Ila kwangu mimi, milioni 5 kwa hali ya sasa siyo kiwango kizuri cha kuanzia, ndiyo maana nimemwambia ukifeli usikimbilie kwa mganga. Kuna post nimesema kwa ni mil 5 basi akiweza kuchanganya na mali kauli itakuwa nafuu. Ningefurahi sana nyie mnaosema ni fedha nyingi mnipe mchanganuo wa kufikirika kwa mwaka wa kwanza. 1. Kodi 2. Leseni 3. Mali anazotakiwa kuanza nazo na bei yake pamoja na usafiri na makario ya faida kwa kila item.4. Mshahara wa mhudumu etc....
 
Kwa ushauri tu chukua hii,maana ndyo mtaji wenyewe na ni vitu viuzika kila siku
Screenshot_20231224-212139_Facebook.jpg
Screenshot_20231224-212139_Facebook.jpg
 
Habari wakuu

Samahani sana Mimi nina mtaji mdogo wa 5m
Ila nahitaji ni fungue hardware itakayo kuwa na vifaa vidogo vidogo vitakavyo endana na bajeti yangu

Naomba kama kuna mtu yoyote mwenye list ya vifaa vya hardware anitumie ili inisaidie kufanya tathimini

Lengo ni kuanza na bajeti ya 5m, kama kuna mtu aliwahi kuanza na mtaji mdogo kama huu naomba anisaidie mawazo
Asanteni.

Anza na cement tu mkuu. Sio lazima uuze kila kitu.
 
Mtaji mkubwa siyo uhakika wa kufanikiwa hata kidogo na wala mtaji mdogo siyo kufeli. Ila kwangu mimi, milioni 5 kwa hali ya sasa siyo kiwango kizuri cha kuanzia, ndiyo maana nimemwambia ukifeli usikimbilie kwa mganga. Kuna post nimesema kwa ni mil 5 basi akiweza kuchanganya na mali kauli itakuwa nafuu. Ningefurahi sana nyie mnaosema ni fedha nyingi mnipe mchanganuo wa kufikirika kwa mwaka wa kwanza. 1. Kodi 2. Leseni 3. Mali anazotakiwa kuanza nazo na bei yake pamoja na usafiri na makario ya faida kwa kila item.4. Mshahara wa mhudumu etc....
Mkuu ndio pesa aliyokua nayo afanyeje kwa hiyo asifanye biashara kisa haijafika unayodhani wewe ndio ipo sawa...la msingi anatakiwa ajue vitu vya hardware atanunua wapi hapo kariakoo tumpe connection za maduka ya Jumla bei nzuri sio kwamba eti 5 m ni ndogo sio kweli mazee...
 
Kwa mtaji huo binafsi nashauri aanze kuspecialize kitu kimoja/viwili hadi mtaji ukue kwanza.

Kuna hardware unaweza kufanya specialisation.
1. Cement, mbao, nondo, misumari, waya wa kench, binding wire.
2. Vifaa vya umeme, kidogo kidogo tu muhimu uwe navyo vyote.
3. Square pipes, hollow sections, rangi za mageti, accessories za welding kama welding rods, discs, bawaba nk.
4.
5.
 
Mtaji mkubwa siyo uhakika wa kufanikiwa hata kidogo na wala mtaji mdogo siyo kufeli. Ila kwangu mimi, milioni 5 kwa hali ya sasa siyo kiwango kizuri cha kuanzia, ndiyo maana nimemwambia ukifeli usikimbilie kwa mganga. Kuna post nimesema kwa ni mil 5 basi akiweza kuchanganya na mali kauli itakuwa nafuu. Ningefurahi sana nyie mnaosema ni fedha nyingi mnipe mchanganuo wa kufikirika kwa mwaka wa kwanza. 1. Kodi 2. Leseni 3. Mali anazotakiwa kuanza nazo na bei yake pamoja na usafiri na makario ya faida kwa kila item.4. Mshahara wa mhudumu etc....
Mkuu kukupa mchanganuo wa faida kwa kila item ni ngumu kwa kuwa biashara ndio kwanza anaanza na pia hata sijui anaweka mkoa gani na eneo gani pia....vitu vingi gerezani havina bei kubwa mkuu hasa kama unaweza kuzunguka na winga mmoja kila bidhaa unayohitaji anakwambia nani ndio muuzaji mkubwa kwa mara ya kwanza baadae unanyooka mwenyewe...nimepoteza contact za wauzaji wakubwa kariakoo ningeweka hapa maana maduka nayajua ntakapohitaji bidhaa itabidi niende maana mimi napofanya ujenzi vitu vingi nafata mwenyewe Gerezani hapo vitu vya 10m vya umeme,bomba na taa za nyumba na holder zake nakua nimemaliza kabisaa na vinakua vingi sasa akifanya uchaguzi kwa 5m au hata 4 m mbona anaenda vizuri maana anachukua contact akijitaji bidhaa sio lazima aende wanakutumia watu wapo kibiashara pana duka moja masink ya vyoo Arusha niliambiwa laki tano kutoka India ila hapo mwenyewe alikua anauza 250,000 mpaka 280,000 biashara inataka ujanja ujanja fulani wa kujua maduka tofauti na bei zake na ubora wa bidhaa pana watu hawasafiri wananunua hapo hapo gerezani na wapo mbali..
 
Back
Top Bottom