Vifahamu viapo vya freemasons kama unataka kuwa mwanachama wao.

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Siku unapoona mwanamume aliyevaa suti ya bei mbaya akipiga magoti gizani, akiwa amefungwa kitambaa machoni na kamba ya kitanzi shingoni, unagundua kuwa Freemasonry si klabu ya kawaida ya matajiri wanaokunywa kahawa na kujadili fursa za biashara.

Ukweli mchungu unaowashtua wengi upo kwenye maneno halisi ya viapo vyao vya siri. Ili kupanda ngazi, mwanachama mpya analazimika kula viapo vinavyobeba maelezo ya kinyama ya adhabu za kimwili endapo atathubutu kufichua siri za chama hicho.

Huu hapa ni uchambuzi wa viapo hivyo vitatu vya msingi:

1. Daraja la Kwanza:
Mwanachama anaweka mkono juu ya kitabu na kula kiapo. Sehemu ya adhabu anayokubali ikitokea amevunja ahadi anatamka:

"...chini ya adhabu ya kukatwa koo langu, ulimi wangu kung'olewa kutoka kwenye mizizi yake, na kuzikwa kwenye mchanga wa bahari..."

2. Daraja la Pili:
Anapopanda daraja, picha inakuwa ya kutisha zaidi. Adhabu inayotajwa hapa ni:

"...chini ya adhabu ya kupasuliwa kifua changu cha kushoto, moyo wangu kung'olewa na kutupwa kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa mwituni..."

3. Daraja la Tatu
Hapa mwanachama anafungwa na kiapo kinachochora picha ya kikatili kabisa:

"...chini ya adhabu ya mwili wangu kukatwa vipande viwili katikati, tumbo na matumbo yangu kutolewa na kuchomwa moto kuwa majivu, kisha kupeperushwa na upepo wa dunia..."

Je una amini Freemasons hutimiza hivi Viapo....!? Hapo swali linabaki kwa wahusika.
Viapo hivi nimevipata kwenye tovuti nyingi zinazo zungumzia haya mambo na wale wafuasi wa zamani wa chama hiki, hukiri.
 
Hana Kitu, Mch Katekela kila siku anazianua Siri zao, anadai alikuwa ofisi moja na Kanumba, wote walihsiwa wasizae watoto
 
Back
Top Bottom